KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Saturday, January 29, 2011

Kuna tenda ya kuzika vichanga-MWananyamala


JESHI la Polisi Nchini, linaendelea kuwasaka waharifu waliohusika katika sakata la kufukia watoto 10 kwa mpigo mbali na kumshikilia Siraji Mburi[45] mhudumu aliyekuwa zamu katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitalini hapo.
Jeshi la polisi linawasaka wazazi wawili mmoja aliyetajwa kwa jina laIdrisa Zuberi kwa kuwa kuonekana kuhusika na uharifu huo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni (RPC) Charles Kenyela, alisema kuwaZuberi anatafutwa na jeshi hilo ka kuwa ripoti ya daktari inaonyesha alikabidhwia mwili wa mtoto wake ukiwa umekufa baada ya mke wake kujifungua mtoto huyo akiwa na matatizo kwa kukosa kiungo cha kutoa haja kubwa.

Kenyela amesema wanamsaka mzazi huyo kwa kuwa haijafahamika alipokabidhwia mwili huoalienda nao ama kuahca hapo kwa kuwapa kazi wahudumu hao.

Hata hivyo imedaiwa kuwa katika uchunguzi wa awali mebaini kuwa wahudumu wa hospitali hiyohususani wale wa kitengo cha kuhifadhia maiti kuchukua tend ya kuzika vichanga vinavyozaliwa mfu hospitalini hapo.

Hata hivyo Kenyela hakuwa tayari kumtaja mtuhumiwa wa pili wa sakata hilo kutokanda na sabau za kipolisi kwa madai kuwa anahofia ataharibu uchunguzi huo

Jeshi hilo bado liko katika uchunguzis kuhusiana na tukio hilo

No comments:

Post a Comment