KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, January 29, 2011

Ajeruhi mke kwa kuombwa fedha ya chakula


GEOFFREY Kimati (30), mkazi wa Kinondoni, amepandishwa kizimbani kwa kosa la kumjeruhi mkewe kwa kiatu baada ya kuomumba fedha ya chakula
Mshitakiwa huyo alipandishwa jana katika mahakama ya Mwanzo Kinondoni akikabiliwa na shitaka hilo la kujeruhi.

Akisoma shitaka hil o Mahakamani hapo,mbele ya hakimu Hanifa Mwingira,Karani Sharifa Dunia alidai kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo Januari 30, mwaka huu katika maeneo ya Leaders.

Alidaiwa kuwa siku ya tukio mshitakiwa aliombwa fedha ya chakula na mkewe, hivyo alikasirika na kuanza kumpiga ngumi na mateke na baadaye kutumia viatu vyake kumjeruhi katika sehemu zake za mwili na kumsababishia maumivu makali.

Hata hivyo mshitakiwa huyo alikana shitaka hilo, alikuwa huru kwa dhamana na kesi hiyo itarudi tena, Februari 17, mwaka huu kwa kutajwa.

No comments:

Post a Comment