KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, January 29, 2011

Kesi ya 'Fisadi Papa' Manji Aleta Rundo la Magazeti




Rundo la magazeti likiletwa mahakamani kama ushahidi wa Manji dhidi ya Mengi Friday, February 04, 2011 11:25 AM
MFANYABIASHARA maarufu nchini, Yusuf Manji (35),

jana aliweza kutoa ushahidi wake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, dhidi ya kukashifiwa na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Ltd, Reginald Mengi kwa kumuita fisadi Papa.
Ushahidi huo ulisikilizwa mbele ya hakimu Aloyce Katemana wa Mahakama hiyo ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Katika ushahidi huo Manji alitoa nyaraka nane zisizo halisi [copy] ambazo ni mialiko ya shughuli za kiserikali ya ndani na nje ya nchi zilizodai kumtaka awe mgeni rasmi na kutoa hotuba mbalimbali za masuala ya kiuchumi.

Mbali na hilo Pia alileta rundo la magazeti ya This Day na Kulikoni yanayochapishwa na katika kampuni ya Mengi pamoja na DVD na kupatikana jumla ya vielelezo tisa vilivyopokelewa mahakamani hapo.

Jana Manji alipanda kizimbani kwa mara ya kwanza kutoa ushahidi huo na kesi hiyo kuonekana kuvuta hisia za watu wengi mahakamani.

Manji aliongozwa na mawakili watatu akiwemo Mabere Marando, Dkt.Ringo Tenga, Richard Rweyongeza, Sam Mapande na Beatus Malima.

Katika ushahidi wake, Manji alidai Aprili 23-27 mwaka 2009, Mengi kwa kutumia kituo cha televisheni cha ITV, alitoa madai kuwa Manji na wafanyabiashara wengine kuwa ni mafisadi papa, wanahamisha rasilimali za taifa kupeleka nje ya nchi na kwamba wameshiriki kikamilifu katika ufisadi wa ununuzi wa magari ya JWTZ, rada, mradi wa makaa ya mawe wa Mchuchuma, mifuko ya hifadhi ya jamii ya PSPF na NSSF, Dowans na Richmond.

Mkanda wa kipindi hicho maalum, ulionyeshwa mahakamani hapo kama kielelezo cha ushahidi.

Hakimu Katemana aliahirisha usikilizaji wa kesi hiyo jana na uhahidi huo unaendelea kutolewa leo asubuhi.

Mengi alimuita mfanyabiashara huyo fisadi papa mwaka juzi katika kipindi chake maalum kilichorushwa na ITV.

No comments:

Post a Comment