KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, January 29, 2011

Kumezuka mapambano Sudan Kusini

Kumezuka mapambano mengine Sudan Kusini, ndani ya jeshi la taifa la Sudan, ambapo watu wasiopungua 30 wamethibitishwa kufariki.


Jeshi la SPLM katika mkutano wa kuleta amani, Rumbek 2005


Mapigano yalianza karibu na mji ulio mpakani wa Malakal katika jimbo la Upper Nile siku ya Alhamisi.

Hii ni baada ya wanajeshi kutoka Sudan Kusini kukataa kusalimisha silaha zao na kupelekwa upande wa kaskazini, kulingana na mkataba wa amani wa mwaka wa 2005.

Mapigano hayo ambayo yalisambaa kwenye maeneo mengine yanatokea kabla ya kutangazwa kwa matokeo ya mwisho ya kura ya maoni iliyofanyika mwezi uliopita ambayo itathibitisha uhuru wa eneo la kusini.

Serikali ya jimbo hilo, ilisema hali katika Malakal kwa hivi sasa ni shuwari.

No comments:

Post a Comment