KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, January 29, 2011

Kesi ya majasusi kutoka Marekani, Iran

Mahakama nchini Iran, inaendesha kesi faraghani ya vijana watatu wa Marekani ambao wanatuhumiwa kuwa majasusi.


Vijana Wamerikani wanaotuhumiwa


Majaji mjini Tehran wamezuwia vyombo vya habari kuripoti kesi hiyo katika kikao cha kwanza.

Wamarekani hao, Shane Bauer, Josh Fattal na Sarah Shourd, walikamatwa mwaka 2009 karibu na mpaka wa Iraq.

Walisema walikuwa wakitalii na waliingia Iran kwa makosa.

Bi Shourd aliachiliwa kwa dhamana, na kuruhusiwa kurudi nyumbani mwaka jana; lakini wenzake wawili bado wamefungwa nchini Iran.

Wakili wao alisema hakuruhisiwa kuonana nao ili kujitayarisha kwa kesi.

No comments:

Post a Comment