KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, January 12, 2011

Kesi ya Mnyarwanda yasikilizwa Ujerumani


Wakimbizi wa Rwanda


Aliyekuwa meya wa Rwanda amefikishwa mahakamani akidaiwa kuamuru matukio matatu ya mauaji ya Watutsi wakati wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, katika kesi ya mwanzo kusikilizwa Frankfurt, Ujerumani.

Onesphore Rwabukombe, Mhutu mwenye umri wa miaka 54 aliyeishi Ujerumani kwa miaka mingi, alikamtwa na polisi wa Ujerumani mwaka jana.

Anashtakiwa kwa mauaji ya kimbari, mauaji na kuchochea mauaji hayo.

Huenda akakabiliwa na kifungo cha maisha iwapo atakutwa na hatia.

Mwendesha mashtaka Christian Ritscher alisoma kupitia hati ya mashtaka akiwa mahakamani, " Kati ya Aprili 11 na 15, 1994, mshtakiwa aliamuru na kusimamia matukio matatu ya mauaji ambapo takriban Watutsi 3,730 waliokimbilia kwenye makanisa kupata hifadhi waliuawa."

Bw Rwabukombe, aliyekuwa meya wa Muvumba kaskazini- mashariki mwa Rwanda, anashtakiwa pia kuhusika binafsi na mauaji yaliyofanywa na wapiganaji wa Kihutu.

Kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa hadi Oktoba.

Takriban watu 800,000 waliuawa wakati wa mauaji ya kimbari ya 1994, wengi wao wakiwa Watutsi.

No comments:

Post a Comment