KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, January 12, 2011

Nundu abaini uozo UBT


Waziri wa Uchukuzi, Omari Nundu, jana aliweza kujionea uozo unaofanyika katika Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo (UBT) baada ya kufika kituoni hapo akijifanya abiria wa kawaida katika ziara yake ya kushitukiza ya kukagua kituo hicho.
Waziri Nundu aliweza kuuziwa tiketi na wapiga debe bila kutambuiliwa na kujionea wapiga debe hao wakifanyqa ulanguzi wa tiketi kwa abiria mbalimbali waliofika kituoni hapo.

Nundu alitinga kituoni hapo akiwa amevalia kawaida kabisa “tisheti na jeans” na hakutambuliwa kabisa na wapiga debe hao hata na badhi ya madereva kutokana na mavazi yake huku wengine walikuwa wakimpa lugha za kihuni kama wanavyowapa abiria wengine wanaofika kituoni hapo.

Katika hali iliyomshangaza ni ile ya mara baada ya kufika kituoni hapo wapigadebe walimgombania kama mpira wa kona huku kila mmoja akitaka kumuzia tiketi.

Hata hivyo waziri huyo alishangazwa na idadi ya wapiga debe kituoni hapo na alishangazwa kuwakuta kwa kwua alishaagiza wapigadebe hao waondolewe kwa kwua wao wameonekanea kuwa kero kwa katika sekta zima ya usafirishaji.

Waziri Nundu aliweza kununua tiketi ya basi linalofanya safari zake Dar-Dodoma na aliweza kubaini uozo mkubwa unaofanywa na mabasi hayo.

Hata hivyo wapiga debe hao waliweza kushtuka baadae walipoona wapiga picha wa magazeti wakimpiga picha na alikuwa akizungumza ndipo walibaini alikuwa waziri huku kila mmoja akishika njia yake na kuondoka eneo hilo.

Hata hivyo Waziri huyo alisema tatizo la wapiga debe linasababishwa na wamiliki wenyewe wa mabasi wka kuwa wameonekana kuwalea na kuagiza kuonana na wamiliki hao

No comments:

Post a Comment