KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, January 12, 2011

Mahakama ya Katiba yaanza kuisikiliza kesi ya Berlusconi,ItaliaMahakama ya katiba ya Italia,Consulta,imeanza kusikiliza kesi iliyo na azma ya kuufafanua uhalali wa kutomshtaki Waziri Mkuu Silvio Berlusconi akiwa kazini.Majaji 15 wanaidurusu sheria mpya ya muda iliyopitishwa mwaka uliopita,inayomuidhinisha Berlusconi na mawaziri wengine kuweza kupewa muda wa miezi 18 kabla ya kushtakiwa.

Endapo kipengee hicho kitabatilishwa,Waziri Mkuu wa Italia Silvio Berlusconi huenda akalazimika kufunguliwa mashtaka katika kesi mbili tofauti za ufisadi na kuepuka kulipa kodi katika biashara yake ya kumiliki shirika la utangazaji la Mediaset.Kulingana na maelezo yaliyochapishwa na gazeti la La Repubblika,majaji wa mahakama hiyo ya katiba wana mitazamo tofauti ila huenda mwafaka ukafikiwa. Akizungumza mjini Berlin hapo jana Jumatano,Waziri Mkuu Silvio Berlusconi amesema kuwa hatua hiyo ni upuuzi mtupu.

No comments:

Post a Comment