KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, January 29, 2011

Waandamanaji waendelea kubaki eneo la Tahrir



Juhudi za kuirejesha Misri katika hali ya kawaida baada ya wiki mbili za maandamano ya kuipinga serikali zimepata pigo, wakati waandamanaji wameendelea kubaki katika eneo la kati katika mji mkuu wa nchi hiyo , Cairo. Serikali imeahidi mageuzi kadha , lakini rais Hosni Mubarak ataendelea kuwa madarakani hadi pale uchaguzi mkuu utakapofanyika Septemba mwaka huu. Rais wa Marekani Barack Obama amesisitiza kuwa Misri haitarejea ilikokuwa.

Waandamanaji wameweka vizuizi na mahema katika eneo la Tahrir wakiapa kuendelea kubakia katika eneo hilo hadi Mubarak atakapoondoka madarakani. Chama kilichopigwa marufuku cha Muslim Brotherhood ni miongoni mwa vyama vya upinzani ambavyo vimekutana na maafisa wa serikali ya Misri, licha ya kuwa mazungumzo yalimalizika kukiwa na maendeleo madogo.Serikali imeridhia mambo mengi, lakini upande wa upinzani umesema kuwa hayakufika umbali wa kutosha

No comments:

Post a Comment