KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, January 10, 2011

Aliyempiga risasi mwakilishi mahakamani

Viongozi wa upande mashtaka nchini Marekani wamemshtaki kijana mmoja mwenye umri wa miaka ishirini na miwili kwa kosa la kumpiga risasi mbunge wa baraza la wawakilishi wa chama cha Demokratic, Gabrielle Giffords, mjini Arizona siku ya jumamosi

Eneo alipopigwa risasi Gabrielle Giffords


Kijana huyo, Jared Loughner, anakabiliwa na mashtaka matano, ikiwemo kujaribu kutekeleza mauaji ya kisiasa na makosa mengine ya mauaji.

Aliyekuwa mchunguzi maalum wa shirika la kijasusi la Marekani William Pickle , ameambia BBC, idadi kubwa ya wajumbe hao wa Congress hawapewi ulinzi wa kutosha kutoka kwa serikali.

Rais Barack Obama leo anawaongoza Wamarekani kukaa kimya kwa muda wa dakika moja, kwa jili ya kutoa heshima kwa watu waliopigwa risasi siku ya Jumamosi mjini Arizona, ambapo Bi Gabrielle Giffords, alijeruhiwa vibaya na yupo mahututi, na watu wengine sita waliuawa.

Bw Obama amesema huu ni wakati wa Wamarekani kuungana pamoja na kuwaweka moyoni wote waliofikwa na janga hilo.

Waendesha mashtaka wamesema wanaushahidi wa kutosha kwamba Jared Loughner, alijiandaa kitambo kufanya kufanya shambulio kama hilo

No comments:

Post a Comment