Kura ya maoni ikiendelea bila vurugu yoyote nchini Sudan, uhusiano kati ya Sudan na Marekani itakuwa sawa, amesema Rais Barack Obama
Rais wa Marekani, Barack Obama
Bw Obama aliliandikia gazeti la New York Times na kusema kuwa iwapo Sudan itatokomeza machafuko nchini humo basi vikwazo vya kiuchumi dhidi ya nchi hiyo vitaondolewa, na pia Marekani itaiondoa Sudan kutoka kwenye orodha ya mataifa yanayofadhili ugaidi.
Lakini kwa upande mwingine, amesema ikiwa vurugu zitaendelea, itamaanisha kuwa Sudan itatengwa zaidi kimataifa.
Alisema macho ya dunia nzima yanaangaalia Sudan na wameungana kwa kusudio la kuhakikisha kuwa pande zote zinazozozana zitawajibika.
No comments:
Post a Comment