KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, January 10, 2011

Wanajeshi 12 wambaka msichana Uganda

Jeshi la Uganda la UPDF limeanzisha uchunguzi dhidi ya wanajeshi wake 12 pamoja na mafisa watatu wa jeswhi hilo kuhusu madai ya ubakaji dhidi ya msichana wa miaka 20 eneo la Karamoja kaskazini mashariki mwa Uganda. Endapo wanajeshi hawa watapatikana na hatia, watanyongwa ama kuhukumiwa kifungo cha maisha

Wanajeshi wa Uganda


Habari za kuanza uchunguzi huo zimekuja baada ya jeshi, kupitia msemaji wake Luteni Kanali Felix Kulaijye, kutangaza mwishoni mwa juma kuwa jeshi limechukua hatua dhidi ya wenzao 12 wanaodaiwa kufanya ubakaji katika kata ya Tapac, tarafa ndogo ya Katikekile, wialya ya Karamoja. Kuhusu kitendo hicho msemaji wa jeshi amekitaja kama lisilo tendo la kawaida.

Ingawa tukio hilo lilitokea mwanzo wa mwaka huu, lakini taarifa zake ndio zimejitokeza hadharani mjin Kampala mwishoni mwa juma .

Taarifa zaidi kuhusu tukio hilo kutoka Karamoja zinaeleza msichana aliyebakwa ambae amelazwa katika hospitali ya Moroto, inadaiwa wanajeshi walimbaka usiku alipokuwa amekwenda kujisaidia. Inadaiwa kuwa walimvizia na kumziba mdomo kwa kutumia viganja vya mikono yao na kumbaka, moja baada ya mwingine kwa kipindi cha saa mbili mfululizo. Inasemekana msichana huyo alikuwa amekewnda kanisani Tapac kuungana na vijana wenzake wengine ambao walikuwa wanasherehekea mwaka mpya.

Baada ya kitendo hicho inasemekana msichana alibaki hoi bila nguvu za kutembea na aligunduliwa na mama mwingine ambae alimsaidia kumpeleka hopitali.

Wanajeshi hao walikuwa katika doria. Msemaji wa jeshi ameongeza kuwa upelelezi umeshaanza na unaongozwa na Luteni Kanali Rugumayo.

Habari zaidi kuwahusu makamanda hao watatu ni kuwa kule sio tu wamesimamshwa kazi lakini pia wamekamtwa. Aidha na habari zaidi kuwahusu wanajeshi 12 waliokamtwa zinaonyesha kama watatu ndio wanaonekana walitenda kitendo hicho ilhali wengine 9 walikamtwa kwa sababu walikuwa pamoja na wale watatu wakati kitendo hicho kilipotokea.

Kitendo hiki ni cha pili kwa muda wa miaka sita. Mwaka wa 2005 wanajeshi watatu walikamatwa kwa kubaka eneo la Kitgum, kaskazini mwa Uganda. Washukiwa walipata hukumu ya kifungo cha maisha.

No comments:

Post a Comment