KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, January 12, 2011

Ajutia kugawa namba ya simu


MWANAMKE mmoja [31] mkazi wa Ukonga Madafu, amejikuta akikosa amani ndani ya nyumba yake kutokana na kitendo chake cha kugawa namba yake ya simu ya mkononi kwa mwanaume anayemfahamu mbele ya mume wake.
Mwanamke huyo jina kapuni amejikuta akikosa raha kutokana na kusumbuliwa na mume wake huyo akimshinikiza kuwa mwanaume huyo alikuwa na mahusiano nae.

Alidai kuwa Januari 12 mwaka huu, akiwa maeneo ya Mwenge aliweza kukutana na mwanaume huyo aliyesoma nae chuo cha CBE miaka minne iliyopita na waliweza kuzungumza na baadae kumuomba namba ya simu ya mkononi na kumpatia bila kumuomba ruhusa mume wake huyo.

Hivyo bila kutambua kuwa mume wake kitendo hicho alikuwa hajakiafiki na waliweza kuagana na wmanaume huyo huku kila mmoja akiahidi kuwa wawe wanawasiliana.

Alidai mara baada ya kuachana na mwanaume Yule mume wake alibadilika na kila anapomsemesha alikuwa hapati majibu sahihi na alikuwa akimjibu vibaya hali iliyomshangaza na hakutambua mume wake alibadilishwa na nini.

Alidai walipomaliza mizunguko yao waliweza kurudi nyumbani na usiku mume huyo alianza kumuuliza maswali kuhusiana na mwanaume aliyempatia namba yake ya simu.

Hata hivyo juhudi za dada huyo kujielezea kwa mume wake hazikuzaa matunda na huku akishinikizwa kuwa Yule alikuwa ni mpenzi wake iweje alikuwa akimsisitiza wafanye mawasiliano.

MWanamke huyo alidai huenda yalikuwa yameisha na mume wake alisubiria kukuche haraka na alipotoka kazini alikwenda kuripoti tukiko hilo kwa kaka wa mke wake akidai alimvunjia heshima na kuongea na mabwana zake mbele yake huku akimtaka shemeji yake amuite na kufanya kikao cha kumuonya.

Hata hivyo dada huyo alionywa na kaka zake wakiwemo na dada zake hali iliyomfanya akose raha na kuonekana anatoka nje ya ndoa kitu ambacho hakikuwa sahihi.

Hadi kufika jana mwanamke huyo alikuwa hajarudishiwa simu yake ya mkononi na simu hiyo alikuwa akitembea nayo mumewe kwa kufanya uchunguzi zaidi wa uaminifu dhidi ya mkewe

No comments:

Post a Comment