KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Wednesday, January 12, 2011
Waislamu Wakasirishwa Maiti ya Kiislamu Kuanikwa Uwanjani Kuagwa
MBALI na masikitiko yaliyotolewa na familia ya marehemu Ismail Omari (25) aliyeuawa katika vurugu za kisiasa zilizotokea Januari 5, mwaka huu mkoani Arusha, waumini wengi wa kiislamu wameonekana kutofurahishwa na kitendo cha kuagwa kwa maiti hiyo.
Watu hao walioweza kuzungumza na NIFAHAMISHE wamesema kitendo hicho si cha kiungwana kilichofanywa na Chama hicho kwa kuwa walikiuka maandiko na maamrisho ya dini ya kiislamu.
Chadema juzi iliwaaga kwa pamoja watu waliofariki katika vurugu katika uwanja wa NMC mkoani Arusha tukio lililoandaliwa na chama hicho.
Mbali na watu hao pia familia ya marehemu huyo ililalamikia kitendo hicho na kudai ilishinikizwa kwa nguvu kupeleka maiti hiyo uwanjani hapo kwa ajili ya kuiaga.
Akizungumza kwa masikitiko baba mzazi wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Omar Juma, alisema walipata shinikizo kutoka kwa chama hicho na kuamriwa kuwa maiti hiyo itawekwa uwanjani ili wafuasi wa chama hicho wapate kuiaga maiti hiyo kwa kuwa marehemu alikufa kishujaa.
Alidai viongozi wa Chadema waliamuru familia hiyo endapo itakataa na kutokukubali kuaga maiti ya ndugu yao chama hicho kitajivua na kujitoa kushughulikia gharama za mazishi na kuifanya familia hiyo kuuacha mwili huo katika chumba cha maiti kwa kuhofia wafuasi wa chama hicho watawadhuru kwa kuwa walifurika katika chumba hicho cha kuhifadhia maiti.
Aliendela kudai kuwa kutokana na sababu hizo familia hiyo ilibaki na masikitiko makubwa kwa kuwa wafuasi wa chama hicho walikuwa wamevalia njuga suala hilo na familia kubaki katika wakati mgumu kutokana na waislamu kuchukukizwa na kitendo hicho na kauli ya viongozi hao.
Hata hivyo Familia hiyo iliomba radhi kwa shehe waliomundaa kwa ajili ya kushughulikia mazishi hayo kwa kupata usumbufu wa kuondolewa katika chumba cha maiti.
Imedaiwa kuwa shehe huyo iliitaka familia hiyo isimuombe yeye msamaha bali iombe msamaha kwa Mwenyezi Mungu.
Watu watatu walipoteza maisha huko mkoani Arusha katika mapambano baina ya wafuasi wa Chadema na Polisi kutokana na kufanya maandamano yaliyozuiwa na jeshi hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment