KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, December 30, 2010

Zimbabwe yakamata wanaopora wageni

Polisi nchini Zimbabwe wamewakamata watu wanane kwa makosa ya uporaji kufuatia mashambulio dhidi ya wafanyabiashara kutoka nje ya nchi yanayofanywa na magenge ya vijana mjini Harare

Rais Mugabe wa Zimbabwe


Vurugu hizo zilianza wakati wafuasi wa Rais Robert Mugabe wakiandamana kupinga kampuni kutoka Afrika Kusini kupewa mkataba wa maegesho ya magari.

Msemaji wa Zanu PF amesema maandamno hayo yalitibuliwa na mahasimu wao wa kisiasa.


Bendera ya Zimbabwe


Mashambulio dhidi ya wageni yanafanyika wakati ghasia za kisiasa zikiibuka kabla ya uchaguzi ambao huenda ukafanyika baadaye mwaka huu.

Mvutano unaanza tena kati ya chama cha MDC na Zanu-PF, ambavyo vimeunda serikali ya muungano miaka miwili iliyopita kufuatia uchaguzi uliokumbwa na dosari na vurugu mwaka wa 2008.

Vurugu

Raia wa Nigeria na China walikuwa miongoni wa wale waliopoteza mali zao ikiwemo simu za mkononi, vifaa vya umeme, na nguo wakati wa vurugu hizo.

Waandishi wa habari wamesema kuwa mamia ya waandamanaji walikuwa wamebeba mabango na baadhi yake yakiwa na maneno ya kuwakejeli watu kutoka ng'ambo.

Mengine yalikuwa yakivishutumu vikwazo aliyowekewa Rais Mugabe na Umoja wa Ulaya, ambavyo vinatarajiwa kupitiwa tena wiki ujao.

Hali ngumu

"Tumewakamata baadhi ya wahalifu na bado tunafanya uchunguzi wa kundi lililojipenyeza kwenye maanadamano hayo," alisema msemaji wa polisi James Sabawu akizungumza na Reuters.

Meya wa Harare, Muchadeyi Masunda, ambaye hana uhusiano wowote na vyama hivyo vikuu, amesema Vurugu za Jumatatu zilionesha hali ngumu ya kiuchumi inayowakablili vijana wa Zimbabwe ambao hawajapata manufaa yoyote kutokana na kuibadilisha sarafu za Zimbabwe kuwa dola.

Makazi

Kwa mujibu wa chama cha MDC, polisi walikamata mamia ya wanachama waliokuwa wameenda kujisalimisha katika kanisa baada ya ghasia kuibuka katika kitongoji cha Mbare mjini Harare, mwishoni mwa juma.

Vijana wa Zanu-PF waliendesha mgomo katika eneo hilo Jumamosi na kupora na kuharibu makazi.

Imeripotiwa kuwa nyumba ya afisa mmoja wa MDC iliteketezwa katika eneo la Bindura, kilomita tisini kaskazaini mashariki mwa Harare.

Katika kauli ya pamoja iliyotolewa na vyama hivyo viwili Jumamosi, walitaka vurugu hizi za kisiasa kukomeshwa.

No comments:

Post a Comment