KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, December 30, 2010

Sudan kuwa taifa jipya

Maafisa wa uchaguzi wamethibitisha matokeo ya kura ya Sudan Kusini kujipatia uhuru

Kusini wachagua kujitawala


Maafisa hao wamesema karibu asilimia 99 ya wapiga kura wametaka nchi hiyo kujitenga na upande wa Kaskazini.

Kura hiyo ni sehemu ya makubaliano ya amani ya mwaka 2005, yaliyomaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miongo miwili.

Ingawa upigaji kura ulifanyika kwa amani, hali ya wasiwasi bado ipo katika maeneo yenye utajiri wa mafuta.

Watu wasiopungua 50 waliuawa mwishoni mwa wiki, katika mapigano baina ya wanajeshi wa jimbo la Upper Nile la Sudan Kusini.

Kujitawala

Mapigano hayo yalitokea kati ya wanajeshi wa Kaskazini, kuhusiana na mzozo wa nani abakie na silaha nzito nzito, wakati vifaa vikihamishwa kuelekea kaskazini katika mpaka mpya.


Karatasi za kura Sudan Kusini


Maafisa wa uchaguzi wamesema asilimia 98.83 ya wapiga kura wa Sudan Kusini wameunga mkono nchi hiyo kujitawala.

Kabla ya tangazo hilo la matokeo mjini Khartoum, rais Omar al-Bashir alisisitiza tena kuwa atakubaliana na matokeo ya kura hiyo.

Omar al-Bashir

"Tunakubali na kuyapokea matokeo hayo kwa sababu yanawasilisha matakwa ya watu wa Sudan Kusini," amesema rais Bashir kupitia televisheni ya taifa.

Mwandishi wa BBC mjini Khartoum anasema Bw Bashir aliwahi kutoa matamshi kama hayo siku za nyuma, lakini tamko hili la kusisitiza litawahakikishia watu wa Kusini walio na mashaka ya kuwa huenda upande wa Kaskazini ukabadili msimamo wake.

Rais huyo amesema ana nia ya kuwa na uhusiano mwema na taifa lijalo la Kusini. Marekani imesema itaiondoa Sudan katika orodha ya nchi inayozituhumu kwa kusaidia ugaidi, iwapo kura hiyo itakwenda salama

wananchi wakishangilia matokeo


Mwandishi wa BBC Nyambura Wambugu akiwa Torit anasema baada ya tangazo kutolewa, wananchi wa huko wametoka nje na kuanza kusherekea kwa kucheza muziki.

"Sasa mimi ni raia wa daraja la kwanza katika nchi yangu" amesema Abiong Nyok, mama wa nyumbani akizungumza na BBC.

Kubaguliwa

Nusu karne iliyopita, raia wa kusini wamepigana vita mara mbili vya wenyewe kwa wenyewe na upande wa kaskazini, ambapo watu zaidi ya milioni mbili wanakadiriwa kufa.

Upande wa Kusini inajiona kama una tofauti za kitamaduni, kidini na kikabila na upande wa Kaskazini, na kusini inaamini imepitia miaka mingi ya kubaguliwa.

Taarifa zinasema kutangazwa na matokeo haya ya mwisho sio mwisho wa mchakato wote.

Changamoto

Masuala yakiwemo eneo la mpakani la Abiyei, uraia, masuala ya kisheria na rasilimali kama vile mafuta, yatahitaji kujadiliwa.

Ingawa ni tajiri kwa mafuta, Sudan Kusini ni moja ya maeneo yenye maendeleo duni zaidi duniani, na mvutano wa kikabila na uhusiano tete na upande wa kaskazini vitaleta changamoto za kiusalama kwa kipindi kirefu.

No comments:

Post a Comment