KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, December 30, 2010

Uingereza yaongeza kodi

Serikali ya Uingereza imetangaza kuwa benki za nchini humo zitatozwa ushuru zaidi ili kuongeza dola milioni 112 katika hazina ya Serikali.


Mitaa yenye benki London


Kodi hiyo ambayo ilitarajiwa kupunguzwa itaanza kutekelezwa kikamilifu, hatua ambao haikutajariwa na benki za Uingereza.

Waziri wa fedha Uingereza George Osbourne amesema kuwa tangazo la ongezeko la ushuru limetolewa kabla ya mabenki kutoa maelezo kuhusu malipo ya ziada.

Pendekezo

Lakini wakurugenzi kutoka benki nne kuu za Uingereza wamekerwa na pendekezo hilo.

Mkataba wa benki kuongeza mikopo kwa wafayabiashara pamoja na kupunguza malipo ya ziada bado haijakamilishwa baada ya mazungumzo na kuhusu mradi wa Project Merlin kugonga mwamba.


Mtaa wa Canary Wharf, wa shughuli za kifedha London


Ikiwa mkataba huo utasainiwa, itamaanisha kuwa benki zitatoa ahadi ya kuweka dola bilioni mia tatu kando, kama mikopo kwa wafanyabiashara kulingana mpango wa serikali wa Benki ya Jamii - Big society Bank.

Kulingana na taarifa iliyotolewa, wakurugenzi wa HSBC, Barclays, Royal Bank of Scotland, na Lloyds watakuwa kwenye kongamano wakiwasiliana kupitia simu na Jumanne alasiri wataamua iwapo wataendelea na mkataba huo.

No comments:

Post a Comment