KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, December 30, 2010

Wengi wamiminika kumuona mwanafunzi mchawi


WAKAZI wa jijini Dar es Salaam waishio karibu na shule ya Liwiti ambayo kuna mwanafunzi anayedaiwa kuwa ni mchawi walimiminika shuleni hapo jana kumshuhudia mwanafunzi huyo.
Mwananfunzi huyo aliyetajwa kwa jina la Rehema aliweza kueleza jinsi anavyofanya shuhuli hizo za uwanga na kuwashangaza wengi ambapo baadhi yao walionekana kuogopa kumsogelea kwa hofu ya kurogwa.

Katika mahojiano shuleni hap akiwa na bibi yake mweanafunzi huyo alikiri kushiriki vitendo hivyo vya ushirikina na kueleza “Kawaida Usiku bibi huwa anakuja ndani kwangu kunichukua na huwa ananipaka mafuta halafu tunakwenda kuwanga kwenye msitu mnene tukiwa nae akinipa maelekezo jinsi ya kufanya”.

Alipoulizwa kuhusiana na walivyomfanya mwalimu huyo alieleza “ tulikwenda nyumbani kwa mwalimu usiku bibi akamtoa dirishani bila kujijua na akaanza kumkaba, kisha tukamuacha, asubuhi ndio alianza kuumwa" alieleza mwanafunzi huyo.

Mwanafunzi huyo amekuwa tishio shuleni hapo kwa kuogopewa na walimu na wanafunzi wenzake kutokana na kushirikiana na bibi yake kwenye mambo ya kishirikina.

Hata hivyo Afisa Elimu, Manispaa ya Ilala, Bi. Tatu Kikwete amesema sakata hilo limethibitishwa ndani ya manispaa hiyo na walipofanya vikao vya ndni waliamua kumsimamisha mwanafunzi huyo masomo yake kwa muda huku uchunguzi wa kina ukiendelea.

No comments:

Post a Comment