KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, December 30, 2010

Grace atakiwa kuondoka mwishoni mwa mwaka


MUME wa Grace amemtaka mke wake huyo ifikapo mwishoni mwa mwaka huu kama hajafanikiwa kushika mimba basi atalazimika aione nyumba chungu kwa kuwa hataweza kuvumilia kuendelea kuishi nae kama mke na mume.


Grace alitamkiwa hayo juzi usiku wakati wakila walipokuwa wakipata chakula cha usiku wakiwa pamoja.

Grace alidai kuwa, wakati wakiwa mezani wakiongea mawili matatu huku wakiwa wanakula chakula cha usiku, ndipo mume wake alimtamkia hivyo na kumwambia azingatie hayo kwani alikuwa hayupo kaitka mzaha.

Grace alipomuuliza ni kwanini aliamua maamuzi hayo mumewe huyo alidai hana mjadala juu ya hilo kwani alishamueleza.

Hata hivyo Grace alimtaka mume wake huyo waende kituo cha afya wakaangalie huenda mmoja wao alikuwa na matatizo lakini mume wake alimjibu yeye ana uhakika hana matatizo anayoyafikiria wka asilimia zote na atamthibitishia hilo.

Alisema mwishoni mwa juma hili ataenda kuripoti tukio hilo kwa wazazi wake

No comments:

Post a Comment