KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, December 30, 2010

Maandamano yaendelea Misri


Maandamano dhidi ya serikali, yameendelea kwa siku ya tano mfululizo mjini Cairo.

Amri ya kutotoka nje ilitangazwa jana usiku katika miji ya Cairo, Alexandria na Suez, baada ya mapambano makali baina ya polisi na waandamanaji.


Waandamanaji mjini Cairo wanataka kiongozi Hosni Mubarak kung'atuka
Hata hivyo, maandamano yameendelea, na jeshi linashika zamu barabarani.

Waandamanaji hasa wamekuwa wakipiga kelele kuwa serikali sio halali, na pia rais Mubarak.

Ni wazi kuwa ahadi aliyotoa rais, kubadili baraza lake la mawaziri na kuleta mabadiliko, hayatoshelezi wananchi.

Wanataraji kuwa, wanaweza kumtoa kiongozi, kama ilivyotokea Tunisia.

Wengi wanasema, baada ya kuishi chini ya sheria ya dharura, inayozuia mkusanyiko wa watu hadharani, sasa wamepata moyo kumiminika barabarani, kutokana na yale yaliyotokea Tunisia.

Watu hawakupata kuonesha nguvu kama hii.

Rais Mubarak amehakikisha kuwa mataifa rafiki ya magharibi yaone kuwa tishio linatoka kwa kundi kubwa la upinzani, la Muslim Brotherhood.

Chama hicho kimepigwa marufuku, na awali kililaumiwa kwa makosa, kuwa kilihusika na maandamano.

Wanaharakati wa kisiasa, wanataka watu wapya wasiohusika na serikali, waruhusiwe kuwania uongozi.

Mohammed El Baradei, aliyewahi kuwa mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Atomiki, ametokeza kuwa kiongozi maarufu wa upinzani.

Lakini wengine wanamtaka Katibu Mkuu wa Jumuiya Nchi za Kiarabu, Jenerali Amr Moussa

No comments:

Post a Comment