KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, December 28, 2010

Wazimbabwe Afrika Kusini wajiandikishe


Maafisa wa serikali ya Afrika Kusini wamewataka raia wote wa Zimbabwe wanaoishi nchini humo kinyume na sheria, watafute vibali vya kuishi katika nchi hiyo kutoka Wizara ya Uhamiaji, kabla ya tarehe 31 mwezi wa Desemba.


Ramani ya Afrika Kusini


Serikali ya Afrika Kusini ilikuwa imetoa muda maalum ikiwataka wahamiaji hao kujiandikisha kwa hadhi ya wakimbizi ama sivyo wafurushwe kutoka nchini hiyo.


Zaidi ya raia million moja unusu wa Zimbabwe walimbilia Afrika Kusini, baada ya kukimbia machafuko ya kisiasa na mgogoro wa kichumi nchini mwao na wamekuwa wakiishi nchini humo bila ya vibali

No comments:

Post a Comment