KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, December 2, 2010

Watu 47 Dar watiwa mbaroni kwa ujambazi


Hussein Kauli

WATU 47 wanaodaiwa kuwa ni majambazi sugu wanaotumia silaha za moto, wamekamatwa jijini Dar es Salaam.

Habari zinasema watu 17 miongoni mwa hao ni hatari na kwamba waliwahi kupata mafunzo ya kijeshi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi katika Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema watu hao wamekutwa na vitu mbalimbali vyenye thamani ya Sh 130 milioni.

Kamnda Kova alisema mali walizokutwa na watuhumiwa hao ni pamoja na magari 12 yanayosadikiwa kuwa ni ya wizi.

Alisema mmoja wa watu hao ambaye ni mkazi wa Kimara Tangi bovu na ambaye anadaiwa kuwa ni jambazi hatari, amekutwa na bastola mbili aina na risasi.

Alisema mtu huyo alikamatwa wakati akitoka kufanya uhalifu.
Kwa mujibu wa kamanda huyo, watu hao 47 wamekamatwa katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam katika msako maalum wa kupambana na wahalifu.

Aliwataka wakazi wa Dar es Salaam kuendelea kushirikiana na polisi katika kuwafichua wahalifu ili wakamatwe

No comments:

Post a Comment