KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Tuesday, December 28, 2010

Wanne mbaroni wakiingiza silaha A.Kusini
Mapambano dhidi ya uharamia Somalia


Polisi nchini Afrika Kusini wamesema watu wanne wameshtakiwa kwa kuingiza silaha nchini humo, zilizokuwa zikielekea katika harakati za kupambana na uharamia nchini Somalia.

Msemaji wa polisi wa Afrika Kusini, amesema, bunduki kumi na tatu zilikutwa katika nyumba moja mjini Durban.

Silaha hizo inaaminika ziliingizwa nchini Afrika Kusini kwa meli iliyotia nanga katika bandari ya Durban.

Polisi bado wanafanya uchunguzi kubaini nani aliyewasaidia watu hao wanne katika harakati hizo za kupata silaha na zilikusudiwa kutumiwa kwa shughuli gani.

Watuhumiwa hao wanne watafikishwa mahakamani siku ya Ijumaa na kwa sasa wapo nje kwa dhamana.

No comments:

Post a Comment