KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, December 28, 2010

CUF yalazimisha maandamano


CHAMA cha Wananchi (CUF) kimeazimia kufanya maandamano ya lazima kushinikiza katiba mpya licha ya Jeshi la Polisi Kanda Maalumu kuzuia maandamano hayo.


Lengo la maandamano hayo kupeleka rasimu ya mabadiliko ya katiba kwa Waziri wa Sheria na Katiba na kufuatiwa na mkutano wa hadhara katika viwanja vya Mnazi Mmoja leo.

Julius Mtatiro Naibu Katibu Mkuu ndani ya chama hicho amesema kuwa, watafanya maandamano hayo kwa lengo hilo la kuwasilisha rasimu hiyo kwa waziri

Licha ya Mtatiro kupata majibu kutoka kwa Kamanda Kova kuwa wamezuia mandamano hayo kwa kuwa barua ya maombi haikuonyesha kama kutakuwa na maandamano licha ya wao kujieleza watateua wachache ili wamfikishie rasimu hiyo Waziri.

Mtatiro amesema hawaoni sababu za msingi jeshi hilo kuzia maandanao hayo na wao walishagharimu zaidi ya shilingi milioni 10 kutangaza maandano hayo.

“Maandamano yapo palepale, nawataka wananchi saa mbili kamili kukutana Buruguni Shell kwa ajili ya kuanza maandamano kuelekea kwa Waziri wa Sheria na Katiba” alisema Mtatiro.

Asubuhi hii, NIFAHAMISHE imeshuhudia askari wa kutuliza ghasia wakizagaa katika barabara ya Uhuru kujiandaa na waandamanaji hao huku wakiwa na silaha na mabomu ya aina mbalimbali.

Katika eneo la Karume, Askari hao waliweza kuwatawanya watu waliowua kwenye vikundi na kurusha risasi huku wananchi wakiwa na hofu kutokana na hali hiyo

No comments:

Post a Comment