KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, December 30, 2010

Wagoma kutaja mali


VIONGOZI wapatao 4,788 wako hatarini kupoteza nafasi zao kazini kwa kugoma kurejesha fomu za kuweka bayana mali zao na madeni yao.
Taarifa hiyo ilitolewa jana jijiji Dar es Salaam na Kamishna wa Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Salome Kaganda wakati alipokuwa akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari.

Kaganda alisema kuwa viongozi hao hadi sasa hawajarejesha fomu ya taarifa kuhusiana na rasilimali pamoja na madeni yao yanayowakabili.

Alisema viongozi hao wakiwemo wa kisiasa na wale wa utumishi wa Umma inafikisha idadi hiyo na kufafanua kwa kufanya hivyo wanaweza wakawa matatani kwa kugoma kutekeleza agizo hilo.

Alisema awali jumla ya fomu zilizotolewa ni 8,410 na zilizorejeshwa ni 3,770.

Hivyo kufuatia hali hiyo ya kutorejeshwa fomu hizo wka viongozi hao hadi kufika sasa viongozi hao watapewa nafasi ya kujieleza na sababu hizo zisipojitosheleza hatua za kimaadili ya utumishi zitafatwa na tarifa zitawasilishwa kwa Rais na nakala atapewa spika wa Bunge la Jamuhuri wa muungano wa Tanzania kwa hatua zaidi

No comments:

Post a Comment