KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, December 30, 2010

Mwanzo wa mwaka, Abood yaua wawili, yajeruhi


WATU wawili wamefariki dunia papo hapo na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria la Kampuni ya Abood kupata ajali.Ajali hiyto ilitokea jana majira ya saa 2 asubuhi eneo la TAMCO Kibaha mkoa wa Pwani wakati basi hilo lilikuwa likitokea mkoani Dar es Salaam kwenda mkoani Morogoro.


Ajali hiyo ilitokea mara baada ya basi hilo kuigonga pikipiki na kuiburuzwa mita zipatazo 500 wakati basi hilo lilipokuwa lkijaribu kuyapita mabasi matatu yaliyokuwa mbele yake na baadae kupinduka na kusababisha majeruhi hao na kuua dereva wa pikipiki hamis Dadi na Lucy ambaye ni mtumishi wa wilaya ya Kibaha kitengo cha ardhi .


Hivyo kutokana na ajali hiyo abiria waliokuwemo ndani ya basi hilo wapatao 51 waliweza kujeruhiwa na kukimbizwa katika hospitali ya Tumbi Kibaha na wengine wanne walikimbizwa Muhimbili

No comments:

Post a Comment