KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, December 30, 2010

Matatizo ya kiufundi zakwamisha noti mpya


IMEDAIWA kuwa matatizo ya kiufundi ndani ya Benki Kuu Ya Tanzania [BOT] imekwamisha utoaji wa noti mpya ambazo zilitarajiwa kuanza kutmika Januari Mosi mwaka huu.
Noti hizo zilitarajiwa kuingia katika mzunguko wa fedha Januari Mosi na zimekwama kutokana na sababu hiyo sababu iliyoelezwa kutoka ndani ya benki hiyo.

Noti hizo tarajio zinatarajiwa kuwa katika sura mpya kw kuweka alama mpya za “GEMINI and SPARK” ndani ya noti hizo na kuwa katika ubora stahili utakakidhi haja za watanzania za zitakuwa na uwezo wa kudumu kwa muda mrefu kuliko awali.

Pia noti hizo za shilingi 500 na 1,000 zitakuwa na waasisi wa Taifa akiwemo Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, na hayati Abeid Amani Karume wa Zanzibar.

Na katika noti za Sh. 2,000, 5,000 na 10,000 zimeendelea kuwa na picha za maliasili za misitu na wanyama wa taifa, na kutakuwa na mabadiliko ya ukubwa katika noti hizo.

No comments:

Post a Comment