KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, December 22, 2010

Ulaya yaunga mkono Sudan Kusini

Afisa mmoja wa ngazi za juu wa serikali ya Uingereza, ameihakikishia serikali ya Sudan kuwa nchi za Magharibi hazioni kwamba kura ya maoni kuhusu kujitawala kwa Sudan Kusini kama ishara ya mgawanyiko wa nchi hiyo.


Raia wa Sudan Kusini


Aliongezea kuwa waziri wa mambo ya kigeni, Bw William Hague, alielezea matazamo huo huo kwa makamu wa rais, Ali Osman Taha, alipokuwa akizungumza naye kupitia simu juma lililopta.

Wakati huo huo Uingereza inatarajia kuwa kura ya maoni itaonyesha raia wengi wanaridhishwa na pendekezo la Sudan Kusini kujitawala.

Aidha, raia wengi kutoka kaskazini mwa nchi hiyo pia wana mtazamo kuwa raia wa Sudan Kusini watataka kujitawala.


Kituo cha kura ya maoni


Afisa huyo wa Uingereza, akizungumza kwa masharti ya kutotajwa jina amesema Uingereza inafanya kila iwezalo kuhakikishia mamlaka nchini Sudan kuwa inaendelea kuiunga mkono.

Amesema huu ni wakati mgumu kwa serikali upande wa kaskazini, ambayo huenda ikapoteza robo ya eneo lake na sehemu kubwa ya mapato yake.

Wakati huohuo Uingereza inajitolea kuisaidia Sudan Kusini, ambayo inakabiliwa na vikwazo kadhaa vya kimaendeleo katika kipindi hiki inapoelekea kupata uhuru wa kijitawala.

Hali hii inatokea wakati Umoja wa Mataifa ukijiandaa kusaidia wakimbizi wa kusini wakiwa kaskazini, iwapo mapigano yatazuka wakati wa kura ya maoni.

Umoja wa Mataifa unajiandaa kusaidia zaidi ya watu milioni mbili wanaokimbia kutoka Kaskazini.

No comments:

Post a Comment