KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, December 22, 2010

Tibaijuka afanya kweli abomoa kuta


WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, jana alianza kazi yake rasmi ya kubomoa kuta alizoamrisha ziblomolewe kwa kuwa maeneo hayo yalichukuliwa isivyo halali.
Jana majira ya usiku, tingatinga la Halmashauri ya Manispaa ya Ilala lilitinga maeneo hayo na kuanza kazi ya kuvunja maeneo ambayo hayo ambayo ni ya wazi na kujengwa bila utaratibu.

Majengo yaliyobomolewa jana ni yale ya kiwanja kilichopo karibu na Hoteli ya Palm Beach, pamoja na ukuta uliojengwa jirani na Hospitali ya Aga Khan katika Barabara ya Ocean Road vyote vikiwa ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Ilala.

Tingatianga lenye namba SM 3937, likiwa chini ya ulinzi mkali, ya askari wapatao 50 wakiwa ndani ya magari yao aina ya Doble Cabin, Toyota Nissa Patrol, huku wengine wakiwa ndani ya mgari Toyota Land Cruiser, tingatinga hilo likifanya kazi yake vilivyo kwa kuangusha kuta hizo huku wakazi wa jiji wakimiminika kuangalia hatua hiyo ya waziri huku wengine wakivutiwa na zoezi hilo.

“ Du huyu mama ndiye waziri ambaye watanzania tulikuwa tunahitaji” safi sana mama” yaani mawaziriwote wangekuwa hivi tanzania ingebadilika, walisema baadhi ya wakazi wa jiji waliokuwa katika zoezi hilo

Huku wengine wakisema “ huyu mama anafaa sana, mna kama pesa na yeye anayo haogopi, bomoa bomoa mma wahidni hao wamezoea kutuonea ndani ya nchi yetu

No comments:

Post a Comment