KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, December 22, 2010

SERIKALI na jamii kwa ujumla imetakiwa kuwasaidia wasioona


SERIKALI na jamii kwa ujumla imetakiwa kuwasaidia wasioona, ili kupunguza idadi ya ombaomba wanaozagaa katika mitaa mbalimbali nchini.

Akizungumza katika warsha ya tathimini ya mradi wa utawala bora, uwazi na uwajibikaji katika uongozi ulioendeshwa na Chama cha Wasioona Nchini (Chawata), mwenyekiti wa chama hicho, Grayson Mlanga alisema serikali na jamii lazima itimize wajibu wake.

Alisema kuwa kushindwa kutimiza wajibu wake wa kuwasaidia wasioona kwa kuwapati elimu kumechochea ongezeko la ombaomba katika mitaa ya miji mingi nchini.

Mlinga aliwaambia washiriki wa warsha hiyo kutoka katika kanda tatu, Kanda ya Ziwa, Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na Kanda ya Kaskazini kuwa ombaomba wengi ni watu wasioona.

“Lakini kwa nini wengine wako mitaani wanaombaomba ili hali wasioona wengine tuko maofisini? Ni wazi kuwa wasioona wakiwezeshwa hasa kielimu wanaweza kuwa kama watu wengine wakatoka mitaani na kujishughulisha na kazi mbalimbali,” alisema mwenyekiti huyo.

Aliaema ikiwa hali hiyo itaachwa iendelee, ombaomba wataendelea kuweko mitaani.

Kwa upande wake mratibu wa mradi huo, Batista Mgumba, alisema kuwa mradi huo ulioanza kutekelezwa na Chawata mwezi Januari mwaka huu, nalenga kuwajengea uwezo viongozi waandamizi wa Chawata kutoka katika matawi ya kanda hizo tatu.

Alisema lengo la mradi huo uliofadhiliwa na Mfuko wa Uadilifu, Uwajibikaji na Uwazi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais ni kuwajengea uwezo viongozi hao ili kuimaRisha utawala bora nchini.

No comments:

Post a Comment