KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, December 14, 2010

Uchaguzi wa KosovoChama cha Democratic Party of Kosovo, PDK kinachoongozwa na Waziri Mkuu Hashim Thaci kimeshinda asilia mia 33 ya kura katika uchaguzi wa bunge uliofanyika Jumapili nchini humo, uchaguzi wa kwanza tangu Kosovo ilipojitangazia uhuru wake kutoka Serbia mwaka 2008. Chama cha LDK, mshirika mkuu wa zamani wa PDK kilipata asilia mia 23.6, katika matokeo yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi nchini Kosovo. Watu milioni 1.6 walikuwa na haki ya kupiga kura, na asilia mia 50 ndio waliojitokeza kupiga kura. Hata hivyo Thaci atakuwa na kibarua kigumu cha kuunda serikali, kwa sababu vyama vikuu vitatu nchini humo vimesema havitaungana na PDK katika serikali ya muungano. Chama cha LDK na vyama vingine vimelalamika kulikuwa na udanganyifu, huku mashirika yasiyo ya kiserikali nchini Kosovo pia yakisema kulitokea udanganyifu wa kura katika maeneo mawili. Mjini Brussels, Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya, Catherine Ashton amewataka wahusika wote waendelee na juhudi za kuunda serikali mpya

No comments:

Post a Comment