KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, December 14, 2010

Cote d`Ivoire yawekewa vikwazo na Umoja wa Ulaya




Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya wanaokutana mjini Brussels, Ubelgiji wamekubaliana kuwawekea vikwazo wafuasi wa Laurent Gbagbo nchini Cote d'Ivore na kumuongezea shinikizo zaidi kiongozi huyo kuachana na madaraka. Cote d'Ivoire imeingia katika mgogoro wa kisiasa kufuatia uchaguzi tete wa rais. Tume ya uchaguzi nchini humo ilimtangaza kiongozi wa upinzani Alassane Ouattara kama mshindi, lakini Gbagbo ambaye bado analihimili jeshi nchini humo na vyombo vya habari vya kitaifa ameng'ang'ania madarakani. Gbagbo ameliteua baraza lake la mawaziri na amesisitiza yeye ndie rais licha ya baraza la usalama la umoja wa mataifa kutoa agizo la kumtaka aondoke madarakani. Wakati huo huo imeripotiwa kuwa makundi mawili hasimu yameshambuliana karibu na hoteli anayokaa Ouattara inayolindwa na Umoja wa Mataifa katika mji mkuu, Abidjan. Wafuasi wa Ouattara wamesema ifikapo Ijumaa wataingia katika majengo ya serikali

No comments:

Post a Comment