KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, December 14, 2010

Sweden inasema iliepuka tukio la kujeruhiwa kwa watu wengi
Waziri wa mambo ya nje wa Sweden amesema nchi yake iliepuka tukio ambalo lingesababisha kujeruhiwa kwa watu wengi zaidi, majeruhi ambayo hayajawahi kushuhudiwa barani Ulaya, kufuatia shambulio la kigaidi lililofanyika nchini humo mwishoni mwa wiki. Akizungumza na shirika la habari la BBC Carl Bildt alisema mripuaji huyo wa kujitoa mhanga alikuwa umbali wa mita chache tu, na dakika kadhaa kutekeleza mauaji ya watu wengi alipojiripua katika eneo moja la kibiashara katika mji mkuu wa Sweden, Stockholm. Mshambuliaji huyo aliyetambuliwa kama Teymour Abdelwahab ndie mtu wa pekee aliyefariki katika shambulio hilo. Watu wengine wawili walijeruhiwa. Waziri Bildt alisema hawana uhakika mshambuliaji huyo alikuwa ana lenga eneo gani, lakini ilionekana alikusudia kuripua mabomu yake katika eneo lililokuwa na watu wengi mjini Stockholm, hasa wakati huu wa msongamano wa watu

No comments:

Post a Comment