Viongozi wa kisiasa Tunisia wanajadili namna ya kuunda serikali mpya ambayo itakuwa mbadala wa uongozi wa Rais Ben Ali. Alikimbilia Saudi Arabia siku ya Ijumaa kufuatia machafuko
Waziri mkuu Ghannouchi akizungumza na kiongozi wa upinzani
Waziri mkuu, Mohammed Ghannouchi anafanya mazungumzo na vyama vya upinzani juu ya serikali ua umoja wa kitaifa.
Msemaji wa upinzani Ahmad Bouzzi wa chama cha Progressive Democratic ameiambia BBC walikuwa wakijadili juu ya muungano wa mpito wa vyama vinne, ikiwemo chama tawala cha RCD.
Uchaguzi wa Rais na wabunge utafanyika kati ya miezi sita hadi saba.
Viongozi wa kisiasa nchini Tunisia wanafanya jitihada ya kujaza nafasi iliyoachwa baada ya Rais Ben Ali kukimbilia Saudi Arabia baada ya ghasia kubwa kufanywa na wananchi.
jeshi la Tunisia wakishika doria mjini Tunis
Wakati huo huo, jeshi la Tunisi linaendelea kushika doria katika miji mikuu ili kuzuia kuibuka upya kwa ghasia.
Televisheni ya taifa ya Tunisia imesema mkuu wa jeshi la usalama wa Rais anatarajiwa kushtakiwa kwa kuchochea ghasia.
Taarifa hiyo imetolewa baada ya serikali ya mpito kusema kuwa inapunguza saa za kutembea usiku kwa saa nne.
Mwandishi wa BBC katika mji mkuu Tunis amesema hii ni ishara kuwa hali inaanza kuimarika nchini humo.
Baada ya ufyatuliaji risasi wa hapa na pale mjini hapo, baadhi ya maduka yamefunguliwa.
Magari mengi ya kibiashara yameonekana mitaani, na wakaazi wamesema vizuizi vya barabarani vimeanza kuondolewa.
No comments:
Post a Comment