KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Thursday, December 30, 2010
Hali ya wasiwasi yatanda Misri
Vifaru havikuwatisha waandamanaji
Ndege mbili za kivita na helikopta ya kijeshi zimeranda katika anga katika eneo la wazi wa Tahrir, mahala ambapo waandamanaji wengi wamekusanyika.
Msururu wa vifaru uliwasili katika eneo hilo, lakini ukazuiwa na waandamanaji.
Wakati huohuo, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton ametoa wito wa kuwepo na "mabadiliko ya utawala yenye utaratibu" nchini Misri.
Bi Clinton ameliambia shirika la habari la ABC kuwa Marekani inataka kuona mabadiliko ambayo yataleta serikali ya kidemokrasia.
"Tunataka kuona uhuru, hatutaki kuona ghasia zinazofanywa na vyombo vya usalama," amesema Clinton.
Vifaru katika mitaa ya Cairo
Waandamanaji hao wanakiuka amri ya kutotembea usiku iliyowekwa.
Mwandishi wa BBC Jeremy Bowen aliyepo kwenye eneo la Tahrir anasema kuna hali ya kutojali baina ya waandamanaji, ambao wanalituhumu jeshi kwa kujaribu kuwatisha.
Kuwasili kwa msururu wa vifaru na milio ya ndege za kivita angani kumezusha hali ya wasiwasi miongoni mwa maelfu ya waandamanaji.
Mapema, licha ya kuwepo kwa magari ya kijeshi, waandamanaji walionekana kama wakiwa na uhuru wakuranda katika eneo la kati la jiji, huku askari wa kuzuia ghasia ambao wamekuwa wakipambana na waandamanaji wakiwa hawaonekani.
Katika wakati mmoja, mwanajeshi mmoja alionekana kubebwa na waandamanaji waliokuwa wakishangilia
Mwanajeshi akiwa amebebwa na waandamanaji
Polisi ambao wamekuwa wakihusika zaidi katika ghasia na mapigano na waandamanaji katika siku za hivi karibuni, hivi sasa hawaonekani tena mitaani.
Mapigano kati ya waandamanaji na vyombo vya dola, hasa polisi wa kuzuia ghasia, yanadaia kusababisha vifo vya watu wasiopungua 100 nchini Misri, tangu kuanza kwa harakati hizi, siku ya Jumanne. Maelfu ya watu wamejeruhiwa baada ya ghasia kuzuka na kufika hadi katika miji ya Cairo, Suez na Alexandria.
Wakati huohuo, matangazo ya shirika la habari la al-Jazeera kupitia mitambo ya satelaiti ya Misri yamesitishwa. Serikali ya Misri mapema iliamrisha shirika hilo la Kiarabu ambalo limekuwa likitangaza maandamanano hayo, kufunga shughuli zake nchini humo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment