KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Friday, December 10, 2010

shairi la Kumtishia Maisha Obama Lamponza


Mwanaume mmoja wa mji wa Kentucky nchini Marekani ametupwa jela miezi 33 baada ya kupatikana na hatia ya kutunga shairi la kumtishia maisha rais wa Marekani, barack Obama.
Johnny Logan Spencer mkazi wa Kentucky nchini Marekani ambaye alitunga shairi la kumtishia maisha rais Barrack Obama wa Marekani, ametupwa jela karibia miaka mitatu kwa kosa hilo, limeripoti gazeti la The Washington Post.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, Johnny Logan Spencer alimuomba radhi Obama kwa kuandika shairi hilo ambalo alikuwa akielezea jinsi Obama atakavyouliwa kwa kupigwa risasi.

Spencer aliliweka shairi hilo linaloitwa "The Sniper," kwenye internet mwaka 2007 na alirudia kuliweka tena shairi hilo kwenye internet mwaka 2009 baada ya Obama kuingia madarakani.

Jaji Joseph H. McKinley Jr. akimsomea hukumu Spencer alimwambia kuwa kwa kutunga shairi la kumtishia maisha rais Obama alikuwa amefanya jambo la hatari sana.

Spencer alihukumiwa kwenda jela miezi 33 na atakapotoka jela atakuwa chini ya uangalizi wa polisi.

No comments:

Post a Comment