KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, December 11, 2010

Liberia yaonya waasi kuhusu Ivory Coast

Rais wa Liberia ameonya waasi wa zamani wa nchi hiyo kutijihusisha na mgogoro wa Ivory Coast.
Rais Ellen Johnson-Sirleaf wa Liberia


Laurent Gbagbo na Allasane Ouattara wanadai kuwa wameshinda urais katika uchaguzi wa mwezi uliopita, na kuzusha wasiwasi mpya wa kutokea ghasia katika nchi hiyo inayozalisha kakao kwa wingi duniani.

Liberia na Ivory Coast ambazo ni nchi jirani, ziliwahi kujihusisha katika mizozo ambayo nchi moja ikipata mtafaruku nchi nyingine hutaka kujihusisha.

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Ivory Coast Choi Young-jin amesema ushindi wa Bw Ouattara "haupingiki".



Laurent Gbagbo na alassane Ouattara


Marekani, Ufaransa na viongozi wa Afrika wamesema Bw Ouattara alishinda uchaguzi na wamemtaka Bw Gbagbo kuachia madaraka.

Uanachama wa Ivory Coast umesitishwa kutoka katika umoja wa kiuchumi wa nchi za Afrika Magharibi Ecowas, mpaka Bw Gbagbo atakapoachia madaraka.

Lakini Marekani imesema Urusi inazuia taarifa ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kumpitisha Bw Ouattara kuwa rais.

Viongozi wote hao wawili waliapishwa siku ya Jumamosi.

Waasi


Waasi wa kaskazini ambao kiongozi wao ni Bw Ouattara wanaendelea kudhibiti eneo la kaskazini, huku majeshi ya serikali yakiwa yanamtii Bw Gbagbo.

Waziri wa habari wa Liberia, Cletus Seah ameiambia BBC kuwa Rais Ellen Johnson-Sirleaf, ametoa onyo kali kwa waasi wa zamani wa Liberia kutojihusisha na mzozo wa Ivory Coast

No comments:

Post a Comment