KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Tuesday, December 14, 2010

Rais Mstaafu Israel Abaka, Jela Miaka Minane

Rais wa zamani wa Israel, Moshe Katsav amepatikana na hatia ya makosa mawili ya kubaka na kunyanyasa kijinsia na pia kutumia wadhifa wake kuzuia sheria kuonyesha makali yake na atahukumiwa kwenda jela kati ya miaka minane na 16.
Rais wa zamani wa Israel, Moshe Katsav mwenye umri wa miaka 65 amepatikana na hatia ya makosa mawili ya kubaka na atatupwa jela kati ya miaka minane na 16.

Majaji watatu wa mahakama ya mji mkuu wa Israel, Tel Aviv walimuona rais huyo wa zamani wa Israel aliyeiongoza Israel kuanzia mwaka 2000 hadi 2007, ana hatia ya makosa ya kubaka, kunyanyasa kijinsia na kutumia wadhifa wake wa urais kuzuia sheria kufuata mkondo wake.

Rais huyo wa zamani alikuwa akituhumiwa kuwabaka na kuwanyanyasa wafanyakazi wake wa kike wakati alipokuwa waziri wa Utalii na wakati alipochaguliwa kuwa rais wa nane wa taifa hilo.

Katsav alimbaka mara mbili mwanamke aliyetajwa kwa jina la "Aleph" wakati alipokuwa waziri wa Utalii na aliwabaka wanawake wengine wawili alipokuwa rais. Alilazimishwa kujiuzulu wadhifa wake na kumuachia mpinzani wake Shimon Peres.

Katsav alikuwa akijitetea kuwa siku zote kuwa hakufanya makosa hayo wakati kesi hiyo iliyochukua mwaka mmoja na nusu ilipokuwa ikiendelea.

Akiongea baada ya hukumu hiyo, Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu alisema "Hii ni siku mbaya kwa taifa la Israel na raia wake, lakini hukumu hii imeonyesha wazi kuwa sheria za nchi zinafuata misingi ya haki".

"Mahakama leo imethibitisha vitu viwili, hakuna mtu aliye juu ya sheria na mwanamke ana haki zote kuhusiana na mwili wake", alisema Netanyahu.

Naye waziri wa ulinzi wa Israel, Ehud Barak alirudia maneno ya waziri mkuu wake kwa kusema kuwa sheria ni msumeno hakuna mtu aliye juu ya sheria.

Kosa la ubakaji huadhibiwa kwa hukumu ya kwenda jela kati ya miaka minne na 16 lakini Katsav ana amepatikana na hatia ya makosa mengine ya kufanya shambulizi la kijinsia na kuzuia haki kutendeka.

Idadi ya miaka ambayo Katsav ataitumikia ndani ya jela itajulikana mwezi januari. Mahakama imeamuru Katsav asalimishe passport yake

No comments:

Post a Comment