KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, December 14, 2010

Mwanamke Aanzisha Vurugu Baada ya Kukataliwa Penzi


Mwanamke mmoja wa nchini Australia amefikishwa mahakamani baada ya kuanzisha vurugu alipokataliwa penzi na dereva taksi.
"Ungemuona mwanamke huyo ungevunjika moyo kidogo, alikuwa ni mnene sana na mwenye sura mbaya, alipoingia ndani ya gari gari yote ilianza kunuka", alisema dereva taksi Dean alipokuwa akihojiwa kuhusiana na kasheshe lililomkuta.

Mwanamke huyo aliingia ndani ya taksi kwenye mji wa Darwin nchini Australia na kumuuliza dereva kama yuko tayari kufanya naye mapenzi.

Dereva alipokataa, mwanamke huyo aliirusha chupa ya bia aliyokuwa nayo na alianza kuishambulia gari hiyo.

"Aliniuliza, Unataka kufanya mapenzi?", alisema dereva taksi Dean mwenye umri wa miaka 41.

"Nilipokataa alianza kunitukana huku akiubamiza mlango wa nyuma na kulishambulia gari langu", alisema dereva huyo wa taksi.

Polisi walimtia mbaroni mwanamke huyo na kumfungulia mashtaka ya kufanya uharibifu wa mali

No comments:

Post a Comment