KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, December 2, 2010

Ouattara "ashinda" urais Ivory Coast

Tume ya uchaguzi wa Ivory Coast imesema mgombea urais wa upinzani Alassane Ouattara ameshinda uchaguzi wa raundi ya pili ya urais, ingawa mahakama ya katiba imepinga matokeo hayo
Alassane Ouattara


Mwandishi wa BBC John James aliyepo mjini Abidjan amesema kutakuwa na mvutano kati ya taaisisi hizo mbili huku matokeo yake yakiwa hayajulikani.

Wafuasi wa rais Laurent Gbagbo walijaribu kupinga matokeo hayo, wakisema kumekuwa na wizi upande wa kaskazini.

Eneo hilo bado limesalia chini ya udhibiti wa waasi wa zamani, anao ambalo Bw Ouattara ana umaarufu mkubwa.Laurent Gbagbo


Uchaguzi huu una lengo la kuiunganisha nchi hiyo ambayo huzalisha kakao kwa wingi zaidi duniani.

Matokeo ya mchuano wa raundi ya pili uliofanyika siku ya Jumapili, yamecheleweshwa sana na kusababisha hali ya wasiwasi nchini humo

Laurent Gbagbo (kushoto) na Alassane Ouattara (kulia)Watu wasiopungua waliuawa siku ya Jumatano usiku katika shambulio kwenye ofisi ya chama cha Bw Ouattara.

Mahakama ya Katiba imesema tume ya uchaguzi kushindwa kutangaza matokeo siku ya Jumatano ina maanisha taasisi hiyi sasa inachukua majukumu.

lakini wakati huohuo tume ya uchaguzi imesema Bw Ouattara ameshinda kwa asilimia 54 ya kura

No comments:

Post a Comment