KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, December 2, 2010

IMEDAIWA kuwa wanaume wasiofanyiwa tohara ni kati ya sababu zinazosababisha kuongeza maambukizi ya ukimwi




Hayo yalijulikana jana katika siku ya maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani ambapo yaliadhimishwa nchini kote.


Imedaiwa kuwa utafiti wa kisayansi uliofanywa umeonyehsa wanaume wengi wasiotahiriwa na kushiriki vitendo vya ngono ni sababu kubwa ya kuongeza maamukizi hayo.


Hivyo kufufatia hayo Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imesema itaanza operesheni maalumu kwa kushirikiana na wadau wengine yakiwemo mashirika ya misaada kutoka Marekani, kufanya tohara ya lazima kwa wanaume katika mikoa ya Mbeya, Iringa, Rukwa, Kagera, Tabora, Shinyanga na Wilaya ya Rorya mkoani Mara.

Hayo yalibainishwa na Waziri wa Wizara hiyo, Dk. Haji Mponda katika siku ya maadhimisho ya siku hiyo

Alisema lengo ni kutaka kupunguza kiwango cha maambukizi ya VVU katika mikoa hiyo ambayo inaon ekana kuwa na viwango vya juu vya maambukizi

No comments:

Post a Comment