KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Thursday, December 2, 2010
Obama: Indonesia ni mfano wa kuigwa duniani
JAKARTA, Indonesia
RAIS wa Marekani, Barack Obama aliyepo nchini Indonesia katika ziara yake ya nchi za Asia ameisifu nchi hiyo na kusema kwamba ni mfano wa kuigwa kwa namna taifa hilo linaloendelea linavyosimaia vyema demokrasia.
Obama ambaye juzi Jumatano alipata fursa ya kuadhimisha mapinduzi yaliyofanyika nchini Indonesia kutoka utawala wa "mkono wa chuma" hadi katika utawala wa kidemokrasia aliimwagia sifa tele nchi hiyo ambayo alikulia akiwa kijana kutokana na imani yao katika kuvumiliana.
Katika hotuba yake ya awali alizungumzia miaka minne aliyoishi nchini humo alipokuwa mtoto na kusisitia umuhimu wa Indonesia ambayo ni taifa kubwa la kiislamu ambalo uchumi ake unakua wka kasi lakini pia watu ake wanaheshimu na kuthamini watu wa dini nyingine.
“Leo nimerejea Indonesia nikiwa kama rafiki, lakini pia Rais ninayetafuta ushirikiano wa ndani zaidi baina ya nchi zetu mbili,” alisema.
Alisema kuwa mabadiliko ya Indonesia yameakisi katika maisha yake, miaka 40 tangu alipoondoka nchini humo, nchi ambayo ina idadi kubwa ya Waislamu duniani, akiwa kijana mdogo, akiwa njiani kuelekea kuwa Rais wa Marekani.
“Indonesia ni sehemu ya maisha yangu” alisema akimkumbuka marehemu mama yake ambaye aliolewa na mtu wa kutoka Indonesia na kwenda huko na mtoto wake huyo wa kiume mjini Jakarta, ambako alikuwa akirusha vishada, akicheza katika mashamba ya mpunga na kukamata wadudu.
Rais huyo wa Marekani alionyesha uwezo wake wa lugha ya Kiindonesia katika ziara yake hiyo ya saa 19 nchini humo na kushangiliwa sana.
Katika hotuba yake aliyoitoa katika Chuo Kikuu mjini Jakarta, Rais Obama aliwataka Waislamu duniani kufanya kazi kwa pamoja na Marekani kupambana na kundi la kigaidi la al-Qaeda.
Obama amerudia matamshi yake aliyoyatoa mjini Cairo mwaka jana kuwa Marekani haiko vitani na Uislamu na kuzitaka pande zote mbili kutoangalia kwa jicho la shaka na kutoaminiana.
“Sisi sote tunapaswa kuwashinda al-Qaeda na washirika wake, kwa kuwa hawana haki ya kujidai ni viongozi wa dini, na hasa sio dini kuu kama Uislamu,” Obama alisema katika hotuba yake.
Obama alikiri kuwa kazi kubwa bado inapaswa kufanyika kuweza kuyaangalia masuala ambayo yamezusha mvutano baina ya Waislamu na Marekan , ikiwa ni pamoja na mzozo wa Mashariki ya Kati pamoja na vita vinavyoongozwa na Marekani nchini Iraq na Afghanistan
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment