KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, December 2, 2010

Chupi za Mitumba Marufuku Ghana


Nguo za ndani za mitumba zitapigwa marufuku nchini Ghana kuanzia mwezi februari mwakani.
Wapenzi wa viwalo vya ndani vilivyotumika majuu nchini Ghana wana miezi michache ya kununua viwalo vyao baada ya nguo hizo za mitumba kupigwa marufuku nchini humo.

Bodi ya viwango ya Ghana imetangaza kuwa kuanzia mwezi februari mwakani, itakuwa ni kinyume cha sheria kuuza chupi na sidiria zilizotumika ambazo huingizwa nchini humo kama mitumba kutoka nchi za ulaya.

Ghana ilipitisha sheria ya kupiga marufuku mitumba ya nguo za ndani mwaka 1994 lakini ilishindwa kusimamia utekelezaji wa sheria hiyo.

Lakini hivi sasa bodi ya viwango ya Ghana imetangaza kuwa itasimamia kikamilifu utekelezaji wa sheria hiyo kuanzia mwezi februari mwakani.

Wafanyabiashara wa mitumba wamelalamika kuwa ajira zao zitapotea sheria hiyo itakapoanza kutekelezwa mwakani.

Serikali ya Ghana imesema kuwa sheria hiyo ni kwaajili ya kulinda afya za wananchi wake

No comments:

Post a Comment