KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Wednesday, December 15, 2010

Nyerere Akabidhi Kontena la Vitabu Musoma


MBUNGE wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere (Chadema), amefanikiwa kupata kontena moja la vitabu vya masomo ya kuanzia shule ya awali hadi Chuo Kikuu na vitabu hivyo vitasambazwa kwa shule zote za sekondari za kata jimboni humo.
Msaada huo umetolewa na wahisani kutoka nchini Marekani, ambao pia ni marafiki zake na kwamba vitabu ambavyo tayari vimeshawasili mjini Musoma na kuhifadhiwa vikisubiri kusambazwa shuleni, vitapunguza zaidi kama si kuondoa kabisa tatizo la upungufu wa vifaa hivyo.

Nyerere alisema kuwa uongozi wake unataka kuona sekta zote ikiwemo sekta ya elimu zinapata maendeleo makubwa kwa kuwanufaisha zaidi wananchi wa jimbo
hilo na kwamba safari ya kusaka mapinduzi makubwa ya maendeleo ya
kisekta aliyotumwa na wananchi wake imeshaanza.

“Nimepata msaada wa kontena zima lenye futi 20 limejaa vitabu vya aina
mbalimbali kuanzia wanafunzi wa chekechea hadi chuo kikuu. Msaada huu
nimeupata kutoka kwa marafiki zangu huko Marekani.

“Vitabu hivi vitasaidia sana kupunguza tatizo kubwa la uhaba wa vitabu
kwa wanafunzi wetu mashuleni,” alisema.

Kwa mujibu wa mbunge huyo wa Musoma Mjini, vitabu hivyo vitakabidhiwa
mbele ya madiwani wote wa jimbo hilo siku yoyote wiki hii kwa sekondari zote za kata na shule za msingi na kwamba vitabu vya chuo kikuu vitawekwa katika maktaba ya mkoa wa Mara, kwani jimbo wala
mkoa huo hauna chuo kikuu

No comments:

Post a Comment