KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, December 15, 2010

Tibaijuka aamuru kuta zivunjwe


WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka ametoa agizo kuvunjwa kwa kuta zote
zilizojengwa katika maeneo ya wazi ya ufukweni yaliyopo Ocean Road na Palm Beach jijini Dar es Salaam.

Agizo alilitoa jana akiwaamuru viongozi wa Manispaa ya Ilala kutekeleza agizo hilo mara moja wakati wa ziara yake alipotembelea maeneo ya wazi yaliyochukuliwa kiholela.

Waziri Tibaijuka akiwa na ujumbe wake wakiwemo watendaji wakuu wa wizara hiyo, wakuu wa wilaya walitumia usafiri wa daladala kutembelea maeneo hayo.

Akifuata ramani ya mipango miji walipofika kwenye kiwanja namba 59 kilichopo Ocean Road, waziri huyo aliamuru kuvunjwa kwa ukuta uliozungushiwa eneo hilo kwa kuwa ramani inaonyesha eneo hilo kuwa ni la wazi.

Mara bada ya ktuoa amuri hiyo Tibaijuka alitoa agizo kuwa mara bada ya kubomolewa kwa kuta hizo aliwaagiza kuwa maeneo hayo yatengenezwe bustani kwani maeneo hayo ni ya wananchi na si kama walivyojichuklia kiholewa kwa matumizi yao binafsi.

Eneo hilo lilidaiwa kuwa lilimilikishwa kwa Jumuiya Shree Hindu Mandal mwaka 1952 kwa matumizi ya kuchomea maiti.

Pia Tibaijuka aliamuru eneo la Palm Beach pavunjwe kwa kuwa Rais mstaafu wa wamu ya tatu Benjamin Mkapa alishatengua umiliki wa eneo hilo kutoka kwa wamiliki wawili waliojulikana kama Shantaben Patel na G. Patel kwa kuwa eneo hilo lilikuwa na mgogoro, pia kuvunjwa kwa nyumba iliyokuwan ndani ya ukuta huo.


Pia eneo la Msasani Bonde la Mpunga aliona limekaa shabagala na kuitaka serikali kufanya uwezekano wa kuwapa nyumba wakazi hao ili eneo hilo liweze kuwekwa katka mpangilio unaofaa.

Pia eneo la Bonde la Msimbazi alisema linahitaji marekebisho kujenga nyumba ili ziweze kusidia wananchi.

Katika ziara hiyo pia alikuwemo mbunge wa jimbo la Ubungo, John Mnyika, Halima Mdee wa Kawe na kuitaka ziara hiyo kufika majimboni humo kwani kuna viwanja nya wazi vilivyomilikiwa na watu isivyo halali

No comments:

Post a Comment