KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, December 2, 2010

Nitaiweza wizara, mimi sio mpole -NahodhaWAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha, amewatoa hofu wanahabari na wananchi kwa ujumla kwa kile anachohisiwa kuwa hataweza kuongoza wizara hiyo kwa kuwa anaonekana ni mpole.
Aliyasema hay o hayo hivi karibuni alipokuwa akizungumza na watendaji wa wizara hiyo na kufafanua maswali aliyoulizwa na baadhi ya waandishi wa habari kuhusiana na wasiwasi wao huo.

Nahodha alisema, “ Napenda niwatoe wasiwasi ndugu zangu waandishi wa habari waliponiuliza ni vipi nitakabiliana na changamoto za wizara hii? Ka kuwa mimi ni mpole,

Mimi sio mpole kama mnavyokuwa na wasiwasi na mimi, naahidi kutekeleza majukumu yangu niliyopewa na mtukufu Rais na watendaji wasije wakabweteka wakajua mimi ni mpole wataumia” alisema Nahodha.

Jana Waziri huyo aliwataka askari polisi nchini kuhakikisha wanatekeleza wajibu wao kwa kufanya kazi kwa nidhamu ya hali ya juu katika kuwalinda watu na mali zao pamoja na suala zima la utekelezaji wa sheria

No comments:

Post a Comment