KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Thursday, December 2, 2010
Tanzania kuadhimisha miaka 49 ya Uhuru Kesho
KESHO ni siku ya maadhimisho ya sikukuu ya uhuru ambapo Tanzania inadhimisha miaka 49 toka kupata kwa uhuru.
Hivyo wananchi na hasa wakazi jiji la Dar es Salaam, wametakiwa kujitokeza kwa wingi kesho katika Uwanja wa Uhuru kuadhimisha maadhimisho hayo kwa pamoja.
Rai hiyo ilitolewa jana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw.Said Sadik, kuwahimiza na kuwaomba wakazi wa jiji kujitokeza kwa wingi kwenye maadhimisho hayo yanayofanyika kila mwaka Desemba 9.
Sadik alisema kuwa, katika maadhimisho hayo, yatapambwa na vijana wa halaiki na gwaride maalumu la majeshi ya ulinzi na usalama ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Pia yahudhuriwa na viongozi wa dini zote, vyama vya siasa, wazee, viongozi wa serikali, wakuu wa idara za serikali, taasisi na mashirika ya umma.
Pia aliwataka viongozi wa dini kuwahamasisha waumini wao wajitokeze katika maadhimisho hayo kwani uhuru huo ni wa kila mmoja ambaye anaishi Tanzania.
Aidha aliwataka wamiliki wa mabasi kujitokeza kwa wingi kuyaelekeza mabasi yao njia ya kuelekea Uwanja wa Uhuru, ili kufanikisha maadhimisho hayo na kuwapa onyo askari polisi wasikamate magari hayo kutokana na shughuli hiyo ya kitaifa
Abushiri ibn Salim al-Harthi
Abushiri ibn Salim al-Harthi alikuwa kiongozi wa upinzani dhidi ya ukoloni wa Wajerumani katika maeneo ya Pangani na pwani la Tanzania mnamo 1889.
Alikuwa mfanyabiashara na mwenye shamba ya miwa karibu na Pangani. Agosti 1889 aliongoza upinzani dhidi ya utawala wa Shirika la Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki katika eneo la Pangani.
Baada ya miezi ya mapambano ( taz. vita ya Abushiri) alikamatwa na kunyongwa na Wajerumani tarehe 16 Desemba, 1889
Hamed bin Mohammed el Murjebi
Hamed bin Mohammed el Murjebi (1837 – 14 Juni, 1905) amejulikana zaidi kwa jina la Tippu Tip. Alikuwa mfanyabiashara mashuhuri katika Afrika ya Mashariki na Kati wakati wa karne ya 19.
Babake alikuwa mfanyabiashara Mwarabu Muhammed bin Juma, mamake aliitwa Nyaso. Hamed aliingia katika shughuli za biashara tangu umri wa miaka 12 akafaulu katika biashara ya misafara kati ya Zanzibar na Kongo. Alipanga misafara ya mahamali waelfu akipeleka bidhaa kutoka Bagamoyo kupitia Tabora hadi Ujiji kwa Ziwa Tanganyika na ndani ya Kongo. Bidhaa alizobeba alitumia kujipatia pembe za ndovu na watumwa; watumwa walisaidia kubeba pembe za ndovu njia ya kurudi hadi pwani. Hemed alitajirika sana. Athira yake ilipanuka katika Kongo ya Mashariki hadi alitawala eneo kubwa sana.
Hamed akapata jina huko Ulaya kwa sababu alikutana na wasafiri na wapelelezi Wazungu kama David Livingstone, Veney Cameron, Henry Morton Stanley, Eduard Schnitzer (Emin Pascha), Hermann von Wissmann na Wilhelm Junker ambao mara nyingi walipata misaada muhimu kutoka kwake.
Wabelgiji walipoanza kujenga ukoloni wao Kongo walimkuta kama mtawala wa Kongo ya Mashariki wakapatana naye na kumpa cheo cha gavana ya Mkoa wa Chutes Stanley ("maporomoko ya Stanley", leo Kisangani) mwaka 1887 alichoshika kwa miaka michache.
Mabadiliko ya ukoloni yaliharibu biashara yake akarudi Zanzibar 1890/91 alipobaki bila misafari mipya hadi kifo chake mwaka 1905.
Jina lake linajulikana kama mfano kwa mabaya ya biashara ya watumwa iliyoharibu maeneo makubwa huko Kongo kabla ya mwanzo wa ukoloni. Yeye mwenyewe aliona watumwa ni sehemu tu ya biashara yake akitajirika hasa na biashara ya pembe za ndovu.
Hamed bin Mohammed el Marjebi amejipatia nafasi katika historia ya Afrika ya Mashariki kwa kuandika tawasifu au kumbukumbu ya maisha yake yeye mwenyewe. Katika lugha ya Kiswahili ni mfano wa kwanza wa tawasifu. Pia ni mfano wa pekee wa kumbukumbu ya kimaandishi ya matokeo ya siku zile zisizoandikwa na Mzungu lakini ny mwenyeji
Mbegha
Mbegha (pia: Mbega)[1] (* baada ya 1700)[2] ni jina la mtu muhimu katika historia ya Washambaa anayekumbukwa kama mfalme wao au mwene mkuu wa kwanza katika kundi hili. Familia ya watawala iliyoanzishwa naye hujulikana pia kama nasaba ya Kilindi.
Washambaa ni wakazi wa milima ya Usambara katika Tanzania kaskazini-magharibi
Mtoto kigego anayefukuzwa na ukoo
Kufuatana na "Habari za Wakilindi"[3] Mbegha kiasili alikuwa mtoto wa Mwarabu aliyetoka Pemba na kuhamia Kilindi na mke wake Mngulu. Inaonekana ya kwamba waliishi baadaye kati ya Wangulu. Mbegha anakumbukwa kama mtoto kigego aliyetangulia kupata meno ya juu iliyotazamiwa kama ishara baya kati ya makabila mbalimbali na mara nyingi waliuawa. Labda kwa sababu babake alikuwa Mwislamu mtoto aliruhusiwa kuishi lakini baada ya kifo cha wazazi na kakaye alinyimwa urithi wake na nduguye waliomkumbuka kama kigego na kumshtaki kuwa ni mchawi.
[hariri] Mwindaji maarufu
Mbegha aliamua kuondoka katika ukoo uliomkataa akawa mwindaji aliyeishi msituni. Alikuwa stadi sana kwa sababu alikuwa kati ya watu wa kwanza waliotumia mbwa wa kuwinda akampenda hasa mbwa wake Chamfumu. Alipata umaarufu kwa sababu alifaulu kupunguza nguruwe witu waliokuwa tishio kubwa kwa wakulima na mazao kwa hiyo walimheshimu na kumpenda. Vijana walikuja kukaa naye akawafundisha mbinu za uwindaji.
Alisemekana kujua pia mbinu za uganga zilizomsaidia kuwinda, kuwashinda maadui na pia kuponya watu.
[hariri] Kilindi
Baada ya kuondoka katika Ungulu alihamia kwanza Kilindi alipokumbukwa kutokana na babake na pia umaarufu wake kama mwindaji. Chifu wa mji akampatia nyumba akawa rafiki wa mwana wa chifu. Siku moja walipoenda pamoja kuwinda huyu kijana aliuawa na nguruwe mwitu na Mbegha aliona hawezi kurudi Kilindi akiogopa hasira ya chifu akaamua kuhama tena akiongozana na vijana 14 na mbwa zake.
[hariri] Chifu wa Bumbuli
Pamoja na kundi lake walizunguka wakapiga kambi huko Zirai kando la Usambara. Wazee wa Bumbuli wakamkaribisha kuja kwao na chifu Mbogho alimpa binti yake kama mke akampandisha kuwa chifu pamoja naye.
Sifa zake zilisambaa kati ya Washambaa. Wakati ule Washambaa wa Vuga walikuwa na vita dhidi ya Wapare wakaona wapate usaidizi wa Mbegha. Kiongozi wa Vuga akamwendea akamwomba kuhamia kwao na kuwa mwene wao. Mbegha aliomba kibali cha mkwe akaongozana na watu wa Vuga pamoja na mke na shemeji yake.
[hariri] Mwene wa Vuga
Huku Vuga alikaribishwa kwa mapigo ya ngoma kubwa watu wengi wakaju kumkaribisha wakamjengea nyumba alipoingia. Mkewe alikuwa mja mzito tayari akamwandaa kitanda kilichofunikwa kwa ngozi ya simba aliyomwahi kuua safarini kuelekea Vuga. Mtoto aliyezaliwa juu ya ngozi ya simba akapokea jina la Simba akawa mrithi wake wa baadaye akipewa pia jina rasmi la Buge. Kutokana na jina hili watawala wa Vuga waliendelea kutumia cheo cha Simba Mwene [4]. Baadaye huyu mwana wa kwanza alikuwa chifu wa Bumbuli kwa kibali cha baba.
Mbegha aliendelea kuoa mabinti kutoka koo za Washambaa mbalimbali na kuweka wanawe kutoka ndohizi kama watawala na wawakilishi wake juu ya vijiji vya mama zao. Kwa njia hii aliunganisha Usambara na koo za Washambaa na kuweka msingi kwa utawala wa kifalme katika Usambara uliosimamia sehemu kubwa ya Tanzania ya kaskazini kabla ya kuja kwa Wazungu. Watawala wa nasaba yake waliomfuata Vuga waliendelea kuoa wake wengi na kuweka wana wao kama watawala wadogo mahali pa mama.
Mzee Mbegha alipongojeka alikaa pamoja na wazee 5 pekee waliomtunza siku tatu hadi alipoaga dunia. Hao wazee hawakutangaza kifo chake waliendelea kuandaa mazishi na ufuasi wake kimyakimya. Walituma ujumbe kwa Buge - Simba aje haraka babake ni mgonjwa. Mbegha alizikwa katika kaburi ndani ya ngozi ya ng'ombe dume mweusi pamoja na paka mweusi. Buga alipofika alitangazwa mara moja kuwa mwene mpya.
[hariri] Urithi wake
Habari za Mbegha zimehifadhiwa katika masimulizi wa watu na kuandikwa mara ya kwanza na Al-Ajemi mwisho a karne ya 19. Wataalamu wa historia waliokusanya historia ya Usambara tangu wakati wa ukoloni walikamilisha historia ya Al Ajemi kwa habari za kieneo.
Hata Mbegha akikumbukwa kama mfalme wa kwanza wa Washambaa kuna wasiwasi kama yeye mwenyewe alitawala kwelikweli au kama alikuwa tu na athira athira kubwa kama mpatanishi na mshauri wa koo mbalimbali.
Lakini kwa hakika alianzisha nasaba ya Kilindi iliyoungansha na kutawala Usambara pamoja na maeneo jirani hadi ukoloni. Wengine wanaona mtawala kamili wa kwanza alikuwa Buga aliyemwua babu yake Mbogho na hivyo kushika utawala kamili juu ya Vuga na Bumbuli[5]. Mwana wa Buge aliyeitwa Kinyashi alianza kupanusha himaya yake kwa njia ya vita, na mtoto wake Kimweri ye Nyumbai alisimamia kilele cha uwezo wa nasaba hii mnamo 1850 akitawala Usambara, Usegeju, Digo na Bondei pamoja na sehemu za Useguha, Upare na tambarare za Maasai. Hata maliwali wa Pangani na Tanga waliokuwa chini ya Sultani wa Zanzibar walilipa kodi za kuthebitishwa vyeo vyao kwa mtawala wa Vuga.[6]. Baadaye biashara iliyopita bondeni iliongeza utajiri wa machifu wa Mazinde waliofaulu kuvunja kipaumbele wa Vuga baada ya 1860.
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa rais wa kwanza wa Tanzania
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa rais wa kwanza wa Tanzania. Alizaliwa Butiama, mkoani Mara pembezoni mwa Ziwa Nyanza tarehe 13 Aprili, 1922. Alifariki dunia 14 Oktoba, 1999. Aliiongoza Tanzania toka mwaka 1961 hadi mwaka 1985.
Yeye ni mwasisi wa itikadi ya ujamaa na kujitegemea. Kabla ya kuingia kwenye siasa alikuwa ni mwalimu. Kazi hii ndiyo ilimpatia jina ambalo lilimkaa maisha yake yote la "Mwalimu." Mwalimu Nyerere ni kati ya viongozi wachache wa Afrika ambao wameacha madaraka kwa hiyari baada ya kutawala kwa muda mrefu. Alipostaafu urais mwaka 1985 alirudi kijijini kwake Butiama ambako aliendesha shughuli za kilimo. Aliendelea kuwa na athari kubwa katika siasa ya Tanzania hadi kifo chake
Julius Kambarage Nyerere alizaliwa mwaka 1922 ( katika kijiji cha Butiama, wilaya ya Musoma, mkoa wa Mara, Tanzania (wakati ule: Tanganyika). Alikuwa mojawapo kati watoto 26 wa Nyerere Burito, chifu wa kabila la Wazanaki. Alipokuwa mtoto Nyerere alichunga mifugo ya babake; katika umri wa miaka 12 aliingia shule akitembea kilomita 30 hadi Musoma. Baada ya kumaliza shule ya msingi aliendelea kusoma shule ya wamisionari Wakatoliki huko Tabora. Katika umri wa miaka 20 alibatizwa akawa mkristo Mkatoliki hadi mwisho wa maisha yake.
Mapadre wakaona akili yake wakamsaidia kusoma ualimu huko Makerere, Kampala, Uganda kuanzia 1943 - 1945. Makerere akaanzisha tawi la Umoja wa wanafunzi Watanganyika pia amejihusisha na tawi la Tanganyika African Association (TAA). Baada ya kumaliza masomo ya ualimu alirudi Tabora akifundisha shule ya St.Mary´s. Mwaka 1949 alipata skolashipu ya kwenda kusoma kwenye Chuo Kikuu cha Edinburgh huko Uskoti / Uingereza akasoma M.A. ya historia na uchumi(alikuwa mtanzania wa kwanza kusoma katika chuo kikuu cha Uingereza na mtanzania wa pili kupata shahada ya elimu ya juu nje ya Tanzania).
Aliporejea Tanganyika kutoka masomoni, Nyerere alifundisha Historia, Kingereza na Kiswahili katika shule ya St. Francis iliyo karibu na Dar es Salaam. Mwaka 1953 alichaguliwa kuwa raisi wa chama cha Tanganyika African Association (TAA), chama ambacho alikisaidia kukijenga alipokuwa mwanafunzi katika chuo kikuu cha Makerere. Mwaka 1954 alikibadilisha chama cha TAA kwenda katika chama cha Tanganyika African National Union (TANU) ambacho kilikuwa cha kisiasa zaidi kuliko TAA. Ndani ya mwaka mmoja chama cha TANU kilikuwa tayari chama cha siasa kinachoongoza Tanganyika.
Uwezo wa mwl. Nyerere uliwashitua uongozi wa kikoloni na kumlazimisha Nyerere kuchagua kati ya siasa na kazi ya ualimu. Nyerere alisikika akisema kuwa alikuwa mwalimu kwa kuchagua na mwanasiasa kwa bahati mbaya. Alijiuzuru ualimu na kuzunguka nchini Tanganyika kuzungumza na watu wa kawaida na machifu ili kuleta muungano katika mapigano ya uhuru. Pia alizungumza kwa niaba ya TANU katika Trusteeship council na Fourth committee ya Umoja wa Mataifa (UN) huko New York. Uwezo wake wa kimaongezi na kuunganisha watu ulimwezesha kufanikisha Tanganyika kupata uhuru bila umwagaji wa damu. Ushirikiano mzuri aliouonyesha aliyekuwa gavana wa wakati huo bwana Richard Turnbull ulisaidia pia kuharakisha upatikanaji wa uhuru. Nyerere aliingia katika bunge la kikoloni mwaka 1958 na kuchaguliwa kuwa waziri mkuu mwaka 1960. Mwaka 1961 Tanganyika ilipata uhuru wake na tarehe 9/12/1961 Nyerere alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa Tanganyika huru na mwaka mmoja baadae Nyerere alikuwa raisi wa kwanza wa jamhuri ya Tanganyika. Nyerere alikuwa kiungo muhimu katika katika muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutengeneza Tanzania baada ya mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 yaliyomtoa madarakani sultani wa Zanzibar Jamshid bin Abdullah.
Julius Nyerere mzee mnamo 197705.02.1977 aliongoza chama cha TANU katika tendo la kuungana na chama tawala cha Zanzibar ASP na kuanzisha chama kipya cha CCM (Chama cha Mapinduzi) akiwa mwenyekiti wake.
Nyerere aliendelea kuongoza Taifa hadi 1985 alipomwachia nafasi raisi wa pili Ali Hassan Mwinyi. Aliendelea kuongoza Chama cha CCM hadi 1990 na kuwa na athari kubwa katika siasa ya Tanzania hadi kifo chake. Inasadikika kuwa Nyerere alishawishi uteuzi wa Benjamini W.Mkapa kama mgombea wa raisi wa mwaka 1995 na ambaye aliteuliwa kuwa raisi kwenye uchaguzi wa mwaka 1995. Nyerere alikaa muda mwingi kwake Butiama akilima shamba lake. Pamoja na haya alianzisha taasisi yenye jina lake; mwaka 1996 alionekana akiwa mpatanishi wa pande mbalimbali wa vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Burundi. Tar. 14.10.1999 aliaga dunia katika hospitali ya St Thomas London baada ya kupambana na kansa ya damu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment