KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, December 2, 2010

Amuua baba yake akigombea urithi


Joseph Lyimo,
Hanang

MKAZI wa Kijiji cha Basobeshi Wilaya ya Hanang na Polisi mkoani Manyara akituhumiwa kumuua baba yake wa kambo kwa kumchinja shingoni kwa lengo la kurithi mali.

Akidhibitisha habari hizi Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoani Manyara Benedict Msuya alisema tukio hilo, lilitokea Desemba 3, mwaka huu, saa 3:00 asubuhi kwenye kijiji hicho.

Mkuu huyo wa Upelelezi Msuya alisema marehemu ni Uwida Gila (60) ambaye pia ni mkazi wa kijiji hicho.

Alisema siku hiyo marehemu Gila alikwenda kwenye kilabu ya pombe na kunywa na baadaye alizidiwa na kulala hapo.

Alisema mtuhumiwa, ambaye jina lake tumelihifadhi, alifika na kumkuta baba huyo akiwa peke yake na kumchinja shingoni na kitu chenye ncha kali na kusababisha kupoteza maisha.

"Baada ya polisi kupata taarifa tulifika kwenye eneo la tukio na tulimkuta Gila akiwa na hali mbaya na baada ya kubaini amefariki tuliruhusu mazishi yake," alisema Msuya.

Alisema uchunguzi wa polisi unaonyesha kuwa mtuhumiwa huyo, alimuua baba huyo, ili arithi mali zake.


Msuya alisema jeshi hilo, linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili waweze kumfikisha mahakamani mtuhumiwa huyo.

Wakati huo huko, mkazi wa Kijiji cha Gidarudagau kilichopo Mbulu, Kidida Endashi (45) amekutwa amekufa kwenye shimo la kuchimba madini.

Kwa mujibu wa Msuya marehemu Endashi alikuwa amelewa, na kwamba inasadikika kwamba alifariki dunia baada kunywa pombe nyingi.

"Marehemu alikuwa na kawaida ya kunywa pombe aina ya Gongo na siku hiyo alikunywa huku akiwa hajala chakula,"alisema.

Kwa mujibu wa baadhi ya viongozi wa vijiji, kata na hata Wilaya mkoani Manyara wamekiri kwamba wananchi katika maeneo hayo, wamekuwa na tabia za ulevi wa kupindukia

No comments:

Post a Comment