KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, December 2, 2010

Mtoto wa Miaka 14 Anayechinja Watu Kama Kuku


Polisi nchini Mexico wamemtia mbaroni mtoto mwenye umri wa miaka 14 ambaye alikuwa akitumiwa na wauza madawa ya kulevya kuwachinja watu na kuweka picha za miili yao kwenye internet.
Edgar Jimenez au maarufu kwa "El Ponchis" alikuwa akiua watu kwa kushirikiana na dada zake kwa malipo ya dola 3000 kwa kila mtu aliyemuua.

Jimenez pamoja na umri wake kuwa mdogo anatuhumiwa kuwachinja watu wengi na kuzikata sehemu zao za siri kabla ya kuitundika miili ya watu aliowaua kwenye daraja la Cuernavaca, nje kidogo ya mji mkuu wa Mexico, Mexico city.

Jimenez alifanya mauaji hayo kwa kushirikiana na dada zake ambao walitumika kuwalaghai watu waliopangwa kuuliwa.

Akijitetea mbele ya waandishi wa habari, Jimenez ambaye alizaliwa mwaka 1996 nchini Marekani, alisema : "Nimewaua watu watu wanne tu, niliyakata makoromeo yao, sikupenda kufanya hivyo , walinilazimisha nifanye mauji hayo au la wangeniua mimi, niliwachinja tu lakini sikwenda kuitundika miili yao kwenye madaraja".

Jimenez alitiwa mbaroni pamoja na dada yake mwenye umri wa miaka 19 wakati walipokuwa wakijiandaa kupanda ndege kuelekea Marekani kumtembelea mama yao wa kambo.

Vyombo vya habari viliripoti kuwa wakati wanatiwa mbaroni, simu ya Jimenez na dada yake zilikuwa na video za mauaji waliyofanya na picha walizozipiga wakati wakiwatesa watu kabla ya kuwaua.

Taarifa zaidi zilisema kuwa Jimenez alikuwa akitumiwa na kundi maarufu la wasafirishaji wa madawa ya kulevya la "Arturo Beltran Leyva" na alianza kulitumikia kundi hilo tangu alipokuwa na umri wa miaka 12

No comments:

Post a Comment