KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, December 2, 2010

Kivumbi Ivory Coast, Wagombea Wajiapisha Wenyewe Kuwa Marais


Hali ni tete nchini Ivory Coast baada ya wagombea urais nchini humo kuamua kujiapisha wenyewe kuwa marais wa taifa hilo.
Hali si shwari nchini Ivory Coast kufuatia vurugu na vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyokaribia kutokea nchini humo baada ya wagombea urais kuamua kujiapisha wenyewe kuwa marais.

Kizaa zaa kilianza baada ya tume ya uchaguzi kumtangaza mgombea wa kambi ya upinzani, Alassane Ouattara ameshinda uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliofanyika novemba 28.

Lakini mahakama ya katiba iliyafuta matokeo ya uchaguzi katika sehemu za kaskazini mwa nchi hiyo na kumtangaza Rais aliyemaliza muda wake, Laurent Gbagbo ndiye mshindi.

Wakati hali ikiwa tete, Gbagbo alijiapisha mwenyewe kuwa rais na ndipo Ouattara alipoamua na yeye kujipisha kuwa rais.

Umoja wa mataifa, Umoja wa ulaya na umoja wa mataifa ya Afrika unayakubali matokeo ya mgombea wa upinzani kushinda uchaguzi huo.

Rais wa Marekani, Barack Obama, Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy wote walimpongeza Alassane Ouattara kwa kushinda uchaguzi huo na kuntaka rais aliyemaliza muda wake akubali matokeo ya kushindwa kwenye uchaguzi huo.

Rais Laurent Gbagbo anatetewa na jeshi la nchi hiyo wakati Alassane Ouattara analindwa na kupewa tafu na majeshi ya umoja wa mataifa.

Hali imekuwa mbaya zaidi kufuatia vurugu zinazoendelea nchini humo ambazo zimepelekea vifo vya watu 17 hadi sasa.

Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki ameenda nchini Ivory Coast kujaribu kusuluhisha mgogoro huo

No comments:

Post a Comment